Injinia Alphonse Augustino Cherehani: Asimulia vipi alivyopatikana hai siku 3 baada ya kuzama MV Nyerere?
Jina la Injinia Augustine Cherehani lilianza kuvuma katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania siku tatu baada ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake katika ziwa Victoria kati ya kisiwa cha Ukerewe na Ukara. Injinia Augustine Cherehani katika kile kilichowaacha wengi vinywa wazi aliokolewa wakati tumaini la kupata walio hai likiwa limesha malizika. Injinia ambaye ndiye fundi mkuu wa kivuko hicho kilichopinduka Mwezi wa tisa tarehe 20 mwaka wa 2018 na kuua watu zaidi ya 225, alimsimulia mwandishi wa BBC Eagan Salla mkasa mzima. 'Siku kama siku nyingine' Siku ya tukio Injinia anasema ilkuwa siku kama siku nyingine lakini kwao kwa misingi ya usafirishaji ilikuwa siku ya kazi kubwa kwani ilikuwa ni siku ya gulio eneo la Bugorora. Kawaida wakazi wa kisiwa cha Ukara hufurika gulioni kujipatia mahitaji mbalimbali na siku hiyo ilikuwa vivyo hivyo. Kabla ya safari kama kawaida alikagua chombo (MV Nyerere) zikiwemo Injini zake ...