Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SIGARA

Ndege apigwa picha akimpatia kinda kipande cha sigara

Mpiga picha za wanayamapori amepiga picha ya Ndege mmoja aliyekuwa akilisha kinda wake kipande cha sigara kilichobaki baada ya kutumika, katika ufukwe mjini Florida nchini Marekani. Katika ukurasa wa Facebook, Karen Mason amesema aliwaona ndege hao mwezi uliopita. Alisema: ''kama utavuta sigara, tafadhali usiache mabaki ya sigara.'' Taasisi ya kutunza mazingira ya hifadhi nchini Uingereza imesema picha hiyo ''inasikitisha''. Bi Mason alipiga picha nyingine ya kinda akiwa amebeba kipande cha mabaki ya sigara mdomo wake: KAREN MASON Ndege hufanya makosa kuwalisha makinda vipande vya sigara kwa kudhani ni chakula. ''Ndege wengi wana shauku kuhusu vitu ambavyo tunavitupa, na mara nyingi huchunguza kwa kuvijaribu ili kujua kama ni chakula au la,'' msemaji wa taasisi ya kulinda ndege aliiambia BBC. ''inasikitisha, mzazi huyu ameamua kuwa mabaki ya sigara kuwa kitu cha kumlisha kinda wake. ''Viumbe hawa wanajaribu ...