MTEULE THE BEST Shirika la kimataifa linaloshughulikia mizozo - International Crisis Group, ICG limemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, Wafula Chebukati kutolea ufafanuzi kauli aliyotoa kwenye mkutano wa waandishi wa habari Oktoba 18 kwamba ni vigumu kwa uchaguzi mpya wa urais utakaofanyika Oktoba 26 kuwa huru na wa haki, kutokana na mazingira yalivyo kwa sasa. Limemtaka mwenyekiti huyo kuiomba mahakama ya juu kuongeza siku kati ya 30 hadi 45, ili kuruhusu kupangwa kwa tarehe mpya ya uchaguzi bila ya kukiukwa kwa katiba. Shirika hilo limeangazia maamuzi ya mahakama kuu ya Januari mwaka 2012 iliposogeza mbele uchaguzi kwa miezi sita, hatua ambayo ilisaidia kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na haki. Shirika hilo limesema, mahakama ya juu inatakiwa kulipatia upendeleo suala hili la kuongezwa kwa siku za kuandaa uchaguzi, baada ya mwenyekiti wa tume ya IEBC, kukiri mwenyewe kwamba tume yake haiwezi kuthibitisha iwapo kutafanyika uchaguzi wa haki ndan...