Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TANESCO

Tanzania yatia saini ujenzi wa mradi wa umeme unaopigiwa kelele na wanamazingira, Rais Magufuli asema ni mradi wa lazima kwa maendeleo

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Stigler's Gorge ni jambo la lazima. Leo rais wa nchi hiyo John Magufuli ameweka saini na wakandarasi wa mradi huo kutoka Misri wakiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi yao. Hatua hiyo inakuja baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka mto Rufiji ambao unaweza kuzalisha megawati 2,100 kufanyika wakati huo Tanzania ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere. Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa na fedha za watanzania wenyewe kwa kiwango cha dola za kimarekani bilioni 2.9 ambayo ni sawa na takribani shilingi trilion 6.5 za kitanzania. Na kampuni itakayofanya kazi hiyo inatoka Misri. Rais Magufuli amesema kwamba walitumia muda kutafakari kuhusu mradi huu kwa sababu Tanzania imebarikiwa na vyanzo vingi sana vya uzalishaji umeme kama vile maji,gesi asilia,upepo,joto ardhi ,makaa ya mawe pamoja na madini ya urani. Na kufikia uamuzi huo wal...

TANESCO YA OMBA RADHI KWA WATUMIAJI

Shirika la Umeme Tanzania ( Tanesco ) limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua katika mifumo iliyozoeleka . Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA) wa Tanesco, Demetruce Dashin amesema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakiamisha mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine. Bw. Dashina amefafanua kwamba kufuatia taharuki ya tatizo la kimtandao lililotokea jana kupelekea watu kupata shida katika ununuzi wa umeme Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limesema tatizo la kimtandao ambalo lilianza jana kufuatia hitilafu katika mfumo limeshughulikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo wanatarajia kumaliza tatizo hilo ndani ya siku chache. “Jana tulikuwa tunafanya uhamisho wa mfumo wa luku kwende katika ofisi zetu mpya hivyo ikawalazimu ...

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)                                                   TAARIFA KWA UMMA

 SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)                                                   TAARIFA KWA UMMA Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawafahamisha Wateja wake wote na Wananchi kwa ujumla kuwa; TANESCO  imeanza utekelezaji wa  Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kuhusu kubomolewa  kwa Jengo la Ofisi za TANESCO  Makao Makuu, liliopo Ubungo Jijini Dar es salam. Kuanzia Jumatatu Novemba 27, 2017. Ukuta wa mbele ya jengo umesha vunjwa ,  pia  baadhi ya Watumishi wa Shirika wameanza kuhamishiwa katika Ofisi nyingine za TANESCO zilizopo jijini Dar es salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama  zaidi. Uongozi w...