MTEULE THE BEST Zuma atakiwa kujibu mashtaka ya rushwa Afrika Kusini Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imewasilishwa na Rais Jacob Zuma kupinga kufufuliwa kwa mashtaka ya ulaji rushwa dhidi yake. Bw Zuma na maafisa wengine wakuu serikali walikuwa wametuhumiwa kupokea mlungula wakati wa ununuzi wa ndege za kivita, maboti ya kushika doria na silaha nyingine. Kuna jumla ya mashtaka 783 kuhusiana na mkataba huo wa mwaka 1999 wa ununuzi wa silaha za mamilioni ya dola. Zuma adaiwa kusinzia bungeni Jacob Zuma : Siogopi kufungwa jela Mashtaka hayo yaliwasilishwa mara ya kwanza dhidi ya Bw Zuma mwaka 2005 lakini yakaondolewa na waendesha mashtaka mwaka 2009 na kumuwezesha Bw Zuma kuwania urais. Hata hivyo, mwaka jana, Mahakama Kuu mjini Pretoria iliamua kwamba kiongozi huyo anafaa kujibu mashtaka hayo. Bw Zuma baadaye aliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Juu ya Rufaa kupinga hatua ya kufufuliwa kwa mashtaka hayo. Rais huyo amekuwa akisisitiza kwamba ...