Alexi Sanchez Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameorodheshwa miongoni mwa makocha wanaotarajiwa kumrithi Mkufunzi wa Chelsea Anonio Conte mwishoni mwa msimu huu huku aliyekuwa beki wa Cheslea Juliano Belletti akiwa mkurugenzi wa kandanda. (Star) Na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasakwa na klabu ya Paris St-Germain. (Mirror) Kiungo wa kati wa Brazil Malcom Tottenham inatarajiwa kuishinda Arsenal katika kumsajili mchezaji wa Brazil na Bordeaux mwenye umri wa miaka 20 Malcom. (Telegraph) Huenda mkataba haujaafikiwa lakini Mkufunzi wa Manchester Pep Guardiola ameipongeza Manchester United kwa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez, 29. (Talksport) Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola Manchester City ilijiondoa katika harakati za kutaka kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal huku wakihofia kwamba hatua hiyo itaathiri vibaya udhabiti wa kifedha wa klabu hiyo.(Times - subscription required) Kiungo wa kati wa Ar...