Liverpool wapo tayari kupambana na Manchester City na Manchester United katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 29. (Sunday Mirror)
Pamoja na kutaka kumsajili Sanchez, Manchester United pia wanataka kumsajili Mesut Ozil, 29. (Sunday Mirror)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kuacha kumsajili Antoine Griezmann, 26, kutoka Atletico Madrid mwisho wa msimu na hata Gareth Bale, 28, kutoka Real Madrid, ili amsajili Sanchez na kumpa mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki. (Mail on Sunday)
Manchester United wamempa Alexis Sanchez hadi siku ya Ijumaa kuamua kama anataka kwenda Old Trafford au la, vinginevyo wataachana naye. (Sunday Express)
Manchester United huenda wakalazimika kumlipa wakala wa Sanchez hadi pauni milioni 10 kama sehemu ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Arsenal. (Sunday Telegraph)
Familia ya Sanchez imewasili mjini London kwa ajili ya maandalizi ya mchezaji huyo kuondoka Emirates huku Manchester City wakiwa bado pia wanamfuatilia. (Goal)
Alexis Sanchez atalipwa pauni 60,000 zaidi kwa wiki iwapo ataamua kujiunga na Manchester United badala ya Manchester City. (The Sun)
Liverpool wanamnyatia winga wa Sporting Lisbon Gelson Martins, 22, ambaye bei yake ni pauni milioni 53. (Correio da Manha)
Real Madrid huenda wakawapa PSG Cristiano Ronaldo pamoja na pesa zaidi ili kumsajili Neymar (Cadena SER)
Manchester United wapo tayari kuvunja rekodi ya dunia kwa kutoa euro milioni 500 kumsajili Neymar kutoka Paris Saint-Germain. Real Madrid pia wanamtaka mchezaji huyo kutoka Brazil lakini hawatolipa zaidi ya euro milioni 400. (Le 10Sport)
Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard ameiambia Real Madrid kuwa Manchester United wamepanda dau la kumtaka. (Don Balon)
Manchester United wanapanga kupambana na Chelsea na Juventus katika kumsajili Alex Sandro. (Mirror)
Chelsea wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Denis Suarez, kuziba nafasi ya Mitchy Batshuayi. (Daily Star)
Liverpool bado wana matumaini ya kumsajili Leon Goretzka kutoka Schalke ambaye pia ananyatiwa na Bayern Munich. (Mirror)
Real Madrid huenda wakawapa Liverpool Gareth Bale pamoja na fedha juu ili kumsajili Mohamed Salah. (Don Balon)
Liverpool wapo tayari kulipa pauni milioni 60 ili kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar, 22, lakini klabu hiyo inataka pauni milioni 90. (Sunday Times)
Kiungo wa RB Leipzig Naby Keita anataka kuhamia Liverpool mwezi Januari badala ya mwezi Julai. Bild)
Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anataka kumsajili kipa wa Napoli, Pepe Reina, 35. (Sun on Sunday)
Real Madrid wana imani na meneja Zinedine Zidane na ameambiwa asiwe na wasiwasi na kazi yake. (Marca)
Barcelona wanafikiria kuwauza wachezaji watano zaidi mwezi Januari akiwemo Gerard Deulofeu, 23 ambaye ananyatiwa na Napoli ya Italia. (Sport)
Borussia Dortmund wanakaribia kumsajili beki wa kati wa Basel Manuel Akanji, 22, kwa pauni milioni 19. (Blick)
Manuel Akanji, 22, pia anafuatiliwa na Manchester United. (Kicker)
Meneja wa Nantes Claudio Ranieri amesema kiungo wa Paris St-Germain Lucas Moura, 25, ameamua kujiunga na Manchester United. (Sunday Express)
Manchester City wanataka kumsajili kiungo Boubakary Soumare, 18, ambaye alijiunga na Lille kutoka PSG. (Mail on Sunday)
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na Jumapili njema.
Maoni