Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya RWANDA

Prof: JOYCE NDALICHAKO AMESEMA AFRICA ITAENDELEZWA NA WAAFRICA WENYEWE

mteulethebest Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema wajibu wa kuiendeleza Afrika uko mikononi mwa Waafrika wenyewe huku jukumu la wadau wengine wa Maendeleo ni  kusaidia kukua kwa Maendeleo hayo. Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo Leo katika Mahafali ya Programu za ESAMI yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI jijini Arusha ambapo amesisitiza kuwa  Waafrika wanapaswa kujisimamia wenyewe katika nyanja za Kijamii na Kiuchumi  kwa lengo la kutimiza malengo ya bara hilo. “ Ili Afrika iweze kuendelea lazima ijisimamie yenyewe katika masuala ya kijamii na kiuchumi na hii itawezekana tu kupitia   vijana ambao wameandaliwa  vyema na wakawa tayari kuhakikisha wanaliendeleza bara la Afrika kwa ujasiri bila kuhofia changamoto watakazokutana nazo,” alisisitiza Waziri Ndalichako Kiongozi huyo amesema bara la Afrika linahitaji Viongozi wenye ujasiri, ambao wapo tayari kuhakikisha Afrika inakwenda mbele kiuchumi na Kija...

Victiore Ingabire na Kizito Mihigo waachiliwa huru na rais Paul Kagame Rwanda

Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake kuwaachilia zaidi ya wafungwa 2000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu. Miongoni mwa wafungwa hao waliofaidika na hatua ya rais huyo ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Victoire Ingabire ambaye alikuwa katika kizuizi tangu 2010. Victoire Ingabire alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 kwa kutishia usalama wa serikali na kudunisha mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Amekuwa akiongoza ukosoaji wa rais Paul Kagame huku akiongezea kuwa hukumu yake ilishinikizwa kisiasa. Bwana Kagame amepongezwa kwa kurekebisha uchumi wa Rwanda lakini pia ameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za kibinaadamu. Kuwachiliwa huru kwa bi Ingabire na wafungwa wengine 2,140 kulitangazwa na seriikali kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri. Taarifa ilisema kuwa bwana Kagame aliwaonea huruma chini ya uwezo wake kama rais. Mbali na Ingabire ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alifungwa kwa miaka 10...

Rwanda yapitisha sheria mpya kupambana na uhalifu wa mtandaoni

Bado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi. Bunge nchini Rwanda, Alhamisi lilipitisha sheria ya uhalifu wa mtandaoni yenye nia ya kuisaidia sekta za kiserikali na binafsi kudhibiti uhalifu huo. Bunge la juu lilipitisha muswada na kupeleka kwenye bunge dogo. Bado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi. Sheria inalenga kulinda taarifa za serikali na binafsi na miundombinu dhidi ya uhalifu wa mitandaoni na mashambulizi ya mitandaoni, kwa mujibu wa Wizara ya habari na mawasiliano na Teknolojia ya Rwanda. ''kwa sasa tunashuhudia mashambulizi ya mitandaoni duniani kote. Mashambulizi ambayo yanatishia usalama wa uchumi na usalama wa taifa,'' alieleza Agnes Mukazibera, Rais wa Bunge la Rwanda, baada ya kura. Sheria itaisaidia serikali kufanya uchunguzi vitisho vyovyote na kushtaki dhidi ya vitendo hivyo katika taasisi binafsi na za umma na kuitetea nchi dhidi ya...

Utafiti: Wanawake wa Rwanda na Kenya ndio wataishi muda mrefu zaidi Afrika Mashariki

Wanawake nchini Rwanda na Kenya ndio wanaotarajiwa kuishi muda mrefu zaidi miongoni mwa wanawake na wanaume katika nchi za Afrika Mashariki, kwa mujibu wa takwimu. Umri wa wanawake kuishi Rwanda kwa sasa ni miaka 69.3 na nchini Kenya ni miaka 69.0. Hata hivyo, umri wa kuishi wa wanaume Uganda ndio ulioongezeka zaidi katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, ambapo umepanda kwa miaka 13.5. Nchini Tanzania, umri wa kawaida wa kuishi kwa wanawake kufikia mwaka 2016 ulikuwa miaka 66, ongezeko la miaka 10 ukilinganisha na mwaka 1990 kwa mujibu wa Utafiti wa Mzigo wa Maradhi Duniani mwaka 2016, ulioratibiwa na Taasisi ya Takwimu za Afya na Utathmini. Kwa wanaume, umri wa kuishi ulikuwa miaka 62.6 kufikia mwaka 2016 ukilinganisha na miaka 53.7 mwaka 1990. Kwa kiwango cha kadiri, umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kwa miaka kumi kufikia sasa tangu mwaka 1990. Nchini Kenya, umri wa kuishi kwa wanawake umeongezeka kutoka miaka 62.6 mwaka 1990 hadi miaka 69 mwaka 2016,...

Hatari tano kwa biashara Afrika Mashariki 2018

Kenya inarudi katika hali ya utulivu kisiasa baada ya uchaguzi wa rais uliochukua muda mrefu na uliokumbwa na misukosuko. Hata hivyo changamoto zitaendelea kuwepo mwaka huu kwa mashirika yanayohudumu nchini humo na Afrika Mashariki kwa ujumla. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la kitaalamu Control Risks linalochambua hatari na udhibiti wa hatari za kibiashara na uwekezaji. Daniel Heal ambaye ni mshirika mkuu wa shirika hilo katika kanda ya Afrika Mashariki, amesema "mwaka 2018 ni mwaka wenye matumaini kwa Kenya na Afrika Mashariki. Tayari tumeanza kuona imani ya wawekezaji ikirejea taratibu kufuatia udhibiti wa kisasa Kenya na azma katika miradi mipya ya miundo mbinu Kenya na katika kanda hiyo kwa jumla. Tunatarajia hili kuendelea hadi mwisho wa mwaka huu." Hata hivyo Daniel anasema nchini Kenya, hitaji la kulipa awamu ya kwanza ya mkopo wa fedha za Eurobond ambazo zilikuwa dola milioni 774.8, linapaswa kuishawishi serikali kudhibiti ukopaji na matumizi kabla deni kufi...

Uchunguzi wa chanzo cha mauaji ya kimbari Rwanda wakamilika

MTEULE THE BEST Image caption Rais wa Rwanda,Paul Kagame Majaji wa Ufaransa wamemaliza upelelezi juu ya shambulio la kombora ambalo lilisababisha kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Ofisi ya mwendesha mashitaka sasa wataamua ikiwa waipeleke kesi mbele ya mahakama. Majaji wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba rais wa wakati huo wa taifa hilo, Juvenal Habyarimana. Rwanda nayo inawalaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya kimbari. Upelelezi umesababisha sintofahamu kati ya mataifa haya mawili, kiasi cha Rwanda kuvunja uhusiano wa kidplomasi a na ufaransa mwaka 2006. Uhusiano huo ulirejeshwa miaka mitatu iliyopita