Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NDEGE

Watu kadhaa walijeruhiwa katika ajali ya ndege isiyo na rubani katika mji wa Urusi - Gavana

Ndege hiyo iliyokuwa na vilipuzi iliripotiwa kunaswa na walinzi wa anga Watu kadhaa walijeruhiwa katika ajali ya ndege isiyo na rubani katika mji wa Urusi - Gavana N dege isiyo na rubani ilianguka kwenye jengo la makazi katika jiji la Urusi la Voronezh siku ya Ijumaa, na kujeruhi takriban watu watatu, Gavana wa eneo hilo Aleksandr Gusev alisema kwenye mtandao wa kijamii. Picha zinazodaiwa kupigwa kwenye eneo la tukio zinaonyesha ukuta wa jengo hilo ukiwa umeharibiwa vibaya, labda kutokana na athari. RIA Novosti alitoa mfano wa kampuni inayosimamia jengo hilo la ghorofa akisema majeraha waliyopata watu waliokuwa karibu ni mikato midogo tu. Nyumba kadhaa ziliharibiwa baada ya ndege isiyo na rubani kugonga jengo kati ya orofa ya pili na ya tatu, iliongeza. Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa ndege hiyo isiyo na rubani ilikuwa imebeba vilipuzi na ilinaswa na walinzi wa anga kabla ya kuanguka. Video iliyoshirikiwa mtandaoni, ambayo inadaiwa kuwa ilirekodiwa na shahidi muda mfupi ka...

MAHAKAMA MOJA NCHINI UFARANSA IMEANZA KUSIKILIZA KESI YA KUKU

Ufaransa: Jogoo Maurice afikishwa mahakamani kwa kuwapigia watu kelele anapowika Sambaza habari hii Messeng ambaza habari hii Tw Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha P Image caption Mmiliki wake, Corinne Fesseau, anasema jogoo Maurice anafanya kile majogoo wote wanafanya 'kuwikaa' Jogoo huyu ambaye mmiliki wake amempatia jina la Maurice, amekuwa kero kwa majirani kwa kuwika kila alfajiri na malambuna kumhusu sasa yanajadiliwa katika mahakama moja nchini Ufaransa. Analaumiwa kwa kusababisha kalele na familia moja katika kisiwa cha Oléron huko Ufaransa. Mmiliki wake, Corinne Fesseau, anasema jogoo Maurice anafanya kile majogoo wote wanafanya 'kuwikaa'. Waliomshtaki Maurice na Maurice mwenyewe hawakufika mbele ya mahakama ya mji wa magharibi wa Rochefort siku ya Alhamisi kesi ilipoanza kusikilizwa. Lakini jogoo huyo ambaye amekuwa maarufu kutokana na kesi inayomkabili, amepata uungwaji mkono kutoka kwa wafugaji kuku wengine ambao walikusanyika nje ya mahakama. Haki mi...

Ndege apigwa picha akimpatia kinda kipande cha sigara

Mpiga picha za wanayamapori amepiga picha ya Ndege mmoja aliyekuwa akilisha kinda wake kipande cha sigara kilichobaki baada ya kutumika, katika ufukwe mjini Florida nchini Marekani. Katika ukurasa wa Facebook, Karen Mason amesema aliwaona ndege hao mwezi uliopita. Alisema: ''kama utavuta sigara, tafadhali usiache mabaki ya sigara.'' Taasisi ya kutunza mazingira ya hifadhi nchini Uingereza imesema picha hiyo ''inasikitisha''. Bi Mason alipiga picha nyingine ya kinda akiwa amebeba kipande cha mabaki ya sigara mdomo wake: KAREN MASON Ndege hufanya makosa kuwalisha makinda vipande vya sigara kwa kudhani ni chakula. ''Ndege wengi wana shauku kuhusu vitu ambavyo tunavitupa, na mara nyingi huchunguza kwa kuvijaribu ili kujua kama ni chakula au la,'' msemaji wa taasisi ya kulinda ndege aliiambia BBC. ''inasikitisha, mzazi huyu ameamua kuwa mabaki ya sigara kuwa kitu cha kumlisha kinda wake. ''Viumbe hawa wanajaribu ...

MAPUNDA: Azawadiwa kwa kuturosha ndege

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemkabidhi kiasi cha shilingi milioni 10, Mtanzania ambaye alisababisha Shirika la Ndege la Tanzania kuwa na ndege ya kwanza ambaye anafahamika kwa jina la Mapunda. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. Rais Magufuli ametoa zawadi hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mapokezi ya ndege ya kwanza Afrika aina ya Air Bus A220-300 ambapo alimpongeza Mzee Mapunda kwa kuhatarisha maisha yake pindi alipokuwa angani akirejea Tanzania baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika ambao ndio walikuwa wamiliki wa ndege hizo. Aidha katika mkutano huo Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Uchukuzi, Isaac Kamwelwe kuhakikisha Mapunda na mkewe wanasafiri bure kwenye ndege za ATCL katika safari zake zote. " Kikubwa ninawaomba watanzania tuwe wazalendo, Mapunda asingekuwa mzalendo leo tusingekuwa na ndege, ninawaomba ATCL mumsafirishe bure mzee Mapunda kwa kazi kubwa aliyoifanya ." amesema Rais Ma...

NDEGE YA TANZANIA AIR-BUS A220 YATUA ACCRA, KUTUA KESHO DAR ES SALAAM

Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania imewasili Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini. Ndege hiyo itawasili kesho majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.   Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege. Balozi Mboweto wafanyakazi na baadhi ya abiria waliokuwapo katika uwanja huo wameonesha shauku kubwa ya kutaka kuiona ndege hiyo ambayo ni ya kwanza kutua Barani Afrika tangu kampuni ya Air-Bus ianze kutengeneza ndege za kizazi cha A220.   “Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona T...

Ndege mpya itakayonunuliwa na Tanzania ni ndege ya aina gani?

Airbus A220-300 Ndege mpya ambayo itakuwa ya karibuni zaidi kununuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege la Air Tanzania inakaribia kukamilika kutengenezwa. Ndege hiyo, ambayo inaundwa na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Airbus, itakuwa ya muundo wa A220-300. Ndege hiyo itakuwa na jina la Dodoma, mji mkuu rasmi wa Tanzania. Serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa kuhamishia shughuli zake zote jijini Dodoma. ADVERTISEMENT Tanzania iliponunua ndege ya majuzi zaidi, 787-8 Dreamliner ya kampuni ya Boeing, ndege hiyo ilipewa jina la Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika. Sawa na ndege hiyo ya Dreamliner, ndege hiyo mpya ya Airbus ina nembo ya 'Hapa Kazi Tu' chini ya jina Dodoma. Hapa Kazi Tu imekuwa kauli mbiu ya Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli tangu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015. Kampuni ya Airbus Alhamisi iliandika ujumbe kwenye Twitter: "Kiwango cha joto ni chini ya sifuri hapa Mirabel, Canada lakini tw...

Ndege mpya inawezaje kuanguka

Lion Air: Haki miliki ya pichaBOEINGImage captionNdege aina ya Boeing MAX 8 ilikuwa imehudumu chini ya mwaka mmoja Ndege ya shirika la Lion Air iliyoanguka baharini, ikiwa na abiria karibu 190 muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu wa Jakarta nchini Indonesia imeendelea kuvutia hisia mbali mbali. Ndege hiyo aina ya Boeng 737 MAX 8, ilikua mpya. Hii ni ajali ya kwanza kuhusisha ndege aina hiyo. Maelezo kuhusu nini hasa kilitokea yamekua finyu lakini chanzo cha ajali hiyo kitajulikana baaada ya uchunguzi kufanywa. Ajali ya ndege mara nyingi husababishwa na mchanganyiko wa mambo tofauti ikiwa ni pamoja na hitilafu ya kimitambo au makosa ya kibinadamu-lakini je ndege mpya inawezaje kuanguka? Ndege hiyo ya Boeng 737 MAX 8 iliyohusika katika ajali siku ya jumatatu ilikuwa imehudumu kutoka mwaka Agosti 15 mwaka 2017 Kwa mujibu wa mkuu wa tume ya kitaifa ya usalama wa uchukuzi wa angani Soerjanto Tjahjano ndege hiyo ilikua imesafiri kwa saa 800. Inasemekana rubani aliomba w...

Boeing 787-8 Dreamliner: Mambo matano makuu aliyoyasema Magufuli kuhusu ndege mpya ya Tanzania

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Jumapili aliongoza taifa hilo kupokea ndege mpya ya kisasa ambayo imenunuliwa kwa ajili ya kutumiwa na shirika la ndege la taifa hilo. Ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ilinunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL). Bei ya ndege hiyo inakadiriwa kuwa $224.6 milioni (Sh512 bilioni za Tanzania) kwa mujibu wa taarifa kwenye tovuti ya kampuni ya Boeing. Ndege hiyo iliwasili majira ya saa 11:10 jioni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kisha kupewa heshima ya kumwagiwa maji na baadaye Rais Magufuli akiwa na viongozi wakuu walioambatana naye akaizindua rasmi. Aidha, yeye na Makamu wake Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, waliikagua kwa kuingia ndani ya ndege ili kujionea mandhari ya ndani. Mataifa ya Afrika yaliyo na Dreamliner Ethiopia (Ethiopian Airlines )*- 19 Kenya (Kenya Airways) - 8 Morocco ...