Donald Trump ashutumiwa kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya wabunge wa Democratic Rashida Tlaib (kati), akiwa na Alexandria Ocasio-Cortez (kushoto) na Ayanna Pressley (kulia) Rais wa Marekani Donald Trump ameshutumiwa kwa ubaguzi wa rangu baada ya kundika ujumbe kwenye twitter akiwashambulia wabunge wanawake wa chama cha Democratic. Amedai kuwa wanawake hao "wamewasili kutoka mataifa ambayo serikali zake ni majanga matupu", kabla ya kupendekeza "warudi walikotoka". Baada ya hapo alisema kuwa spika Nancy Pelosi "atafurahi sana kuwashughulikia kwa haraka mipango ya safari ya bure". Haya ni wiki moja baada ya Bi Pelosi kukabiliana kwa maneno na "kundi hilo", la wabunge wasio watu weupe wa mrengo wa kushoto wa chama cha Democratic. Kati ya wabunge hao wanne, watatu - Alexandria Ocasio-Cortez, Rashida Tlaib na Ayanna Pressley - walizaliwa na kulelewa Marekani, huku wanne, Ilhan Omar, alihamia Marekani alipokuwa mtoto. Bi Ocasio-Cortez alizal...