Tanzania sasa itahitajika kuwafunga Uganda na kuomba Lesotho wafungwe na Cape Verde ili wao wafuzu Ndoto za Tanzania kushiriki mashindano ya kandanda kwa timu za taifa bara la Afrika (Afcon) zimekumbana na dhoruba kali. Timu ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars hapo jana jioni, Novemba 18 ilihitaji alama tatu dhidi ya Lesotho ili kufuzu katika fainali hizo zitakazopigwa mwakani Cameroon kwa mara ya kwanza toka mwaka 1980. Stars inayonolewa na nyota wa zamani wa Nigeria Emmanuel Amunike iliingia dimbani huku mashabiki wake wakiwa na Imani kubwa juu ya timu yao. Laiti Stars ingepata ushindi wa namna yeyote ile wangefikisha alama nane ambazo Cape Verde na Lesotho wasingeweza kuzifikia. Tayari Uganda the Cranes wamefuzu kupitia kundi hilo la L kwa kufikisha alama 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyengine yeyote. Uganda ilifuzu baada ya kuifunga Cape Verde goli 1 bila majibu. Hayo yalikuwa matokeo ambayo Watanzania walikuwa wakiyaombea sababu Cape Verde ilisalia na alama zake ...