Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UTEKAJI

IRAN YALIPIZA KISASI YAKAMATA MELI YA UINGEREZA

Iran yakamata meli ya Uingereza eneo la Ghuba Kutakuwa na 'madhara makubwa''ikiwa Iran haitaachia meli ya mafuta ya uingereza wanayoishikilia, Waziri wa mambo ya kigeni Jeremy Aunt ameeleza. wamilili, Stena Impero kuwa wameshindwa kufanya mawasiliano na meli hiyo. Kamati ya dharura ya serikali hiyo, cobra, anakutana kwa ajili ya kuzungumzia jambo hilo. Bwana Hunt amesema kitendo hicho ''hakikubaliwi kabisa. ''Tunajua wazi kuwa hali hii haitakuwa rahisi kuitatua, kutakuwa na madhara makubwa,'' alisema. ''hatuangalii suluhu ya kijeshi.Tunatafuta suluhu ya kidiplomasia kutatua hali hii, lakini tunajua tunapaswa kushughulikia.'' Amesema wafanyakazi ndani ya meli walikuwa wa mataifa tofauti tofauti lakini hakuna raia wa Uingereza aliykuwa akifahamika kuwa ndani ya chombo hicho. Chombo cha kampuni ya Stena Impero ilikuwa ikisafiri majini ikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London. ''Balozi wetu mjini Tehran anf...

Serikali yagomea wapelelezi wa nje kuchunguza sakata la MO Dewji

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Serikali haiwezi kuruhusu vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nje ya nchi kuchunguza tukio la kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.  Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 16, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari.  Amesema anaamini polisi kuna wataalamu wanaoijua kazi yao, wanaifanya kwa kuzingatia maadili.  “Kuna haja gani kuleta vyombo vya nje wakati tuna jeshi bora na lenye uelewa mkubwa licha ya kukabiliwa na changamoto za hapa na pale,” amesema.  Amesema  polisi hawajashindwa kuchunguza jambo hilo na lipo ndani ya uwezo wao.  Alipoulizwa kuhusu familia ya Mo Dewji kutangaza dau la Sh1bilioni kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo, Masuani amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa si msemaji wa familia. Hata hivyo, amesema wananchi wana nafasi ya kutoa taarifa kwa polisi  ili wawe...