Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ISRAEL

Mashambulio ya angani yakwamisha amani Israel na Gaza

Gaza imeshuhudia mashambulizi zaidi ya angani baada ya roketi kuelekezwa Israel Israel imefanya mashambulio mapya ya angani dhidi ya ngome ya wanamgambo baada ya roketi iloyorushwa kutoka Gaza kuanguka katika eneo lake, hatua ambayo huenda ikalemaza juhudi za kusitisha mapigano. Vyombo vya habari vya Palestina vinasema makombora ya Israel yalilenga maeneo yanayokaliwa na kundi la Kipalestina la Islamic Jihad (PIJ) mapema siku ya Ijumaa, na kuwajeruhi. Hii ni baada ya roketi tano kurushwa katika ardhi ya Israel Alhamisi baada ya PIJ kuitikia wito wa kusitisha mapigano. Ushawishi wa Iran 'unaongezeka' mashariki ya kati Mapigano yalizuka baada ya Israel kumuua kamanda wa PIJ siku ya Jumatatu. Israel ilisema Baha Abu al-Ata alikuwa "mtu hatari"ambaye alihusika kupanga shambulio la roketi la hivi karibuni kutoka Gaza. Zaidi ya maroketi 450 yalirushwa Israel, katika mashambulio kadhaa ya angani yaliyofanywa kutoka Gaza katika muda wa siku mbili . Mzozo kati ya Isr...

Israel: Isaak Hayik avunja rekodi ya mchezaji soka mkongwe zaidi duniani

Haak Hayik mchezaji soka mkongwe duniani Mchezaji wa soka wa Israel, Isaak Hayik aliye na miaka 73 amevunja rekodi ya kuwa mwanasoka mkongwe zaidi duniani. Isaak aliandikisha historia hiyo baada ya kucheza kama mlinda lango wa timu ya Israeli ya Ironi ama Yehuda siku ya Ijumaa. Licha ya umri wake mkubwa, Hayik alisema "yuko tayari kwa mchezo mwingine" baada ya kucheza kwa dakika 90. Amepokea tuzo ya Guinness World Records katika hafla iliyoandaliwa baada ya mechi hiyo, siku kadhaa kabla ya sherehe 74 ya kuzaliwa kwake. Japo timu yake ilifungwa mabao 5-1 na timu ya Maccabi Ramat Gan, mzaliwa hiyo wa Iraq anasemakana kuwa alionesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo. "Hii sio fahari yangu pekee bali ni fahari ya Israel michezoni kwa ujumla," Hayik aliliambia shirika la habari la Reuters. Mmoja wa watoto wake wa kiume Moshe Hayi, aliye na umri wa miaka 36, alisifia ufanisi wa baba yake kwa furaha na bashasha"siamini kwa kweli", alisema. Haki mili...

Rais Magufuli kutuma barua kwa Waziri Mkuu wa Israel

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameandika barua ambayo itapelekwa kwa Waziri Mkuu wa Israel, Israel Benjamin Netanyahu kwaajili ya shukrani kwa kutambua mchango wa taifa hilo kwa Tanzania.   Rais Magufuli amesema hayo leo Novemba 8, alipokutana na timu ya wataalamu wa matibabu ya moyo kutoka nchini Israel na Marekani, Ikulu Jijini Dar es salaam, wataalam hao wanashirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.  "Nimeandika barua ambayo nitakukabidhi Balozi, umpelekee Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu inayoeleza namna ninavyokubali utendaji kazi wake, najua hii barua itamfikia ili kuonesha kazi nzuri mliofanya," amesema Rais Magufuli.  "Niwaombe Madaktari na Wataalamu kutoka Israel mkija msije tu kwa masuala  ya Udaktari siku nyingine mnaweza mkaja kwa masuala ya kufurahi,  mnaenda Serengeti National Park, Ngorongoro na maeneo mengine ambayo ni  ya kuvutia".  Madaktari hao zaidi ya thelathini wamekuja nc...

Israel yasema ubalozi mpya mjini Jerusalem ni Historia

Marekani imeufungua rasmi ubalozi wake mpya katika mji wa Jerusalem huku Wapalestina zaidi ya 40 wakiuwawa na mamia wengine wakijeruhiwa kwenye mapambano na askari wa Israel katika harakati za kuipinga hatua hiyo. Hatua ya Marekani ya kuuhamishia rasmi ubalozi wake kwenye mji  wa Jerusalem kutoka Tel Aviv imetekelezwa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Balozi wa Marekani nchini Israel David Friedman amesema kuwa baada ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa taifa la Israel wakati muhimu kama huu na wa kihistoria ni kwa sababu ya ujasiri wa mtu mmoja tu ambaye ni rais wa Marekani Donald Trump. Rais huyo wa Marekani hakuhudhuria sherehe hizo lakini alitoa hotuba kupitia kwenye Video. Trump amesema Marekani itaendelea kujitolea kikamilifu katika kuuwezesha mpango wa amani wa Mashariki ya Kati. Jared Kushner mkwe wa Trump na mke wake Ivanka binti yake Tru...

Watu 52 wafariki Marekani ikifungua ubalozi mpya Jerusalem

Mamia ya watu wamejeruhiwa, kwa mujibu wa maafisa wa Palestina Raia 52 wa Palestina wameuawa na wengine 2,400 wamejeruhiwa na wanajeshi wa Israeli katika mapigano mabaya kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 2014 katika mpaka wa Gaza, maafisa wa Palestina wanasema. Raia wa Palestina wamekuwa wakiandamana kwa wiki kadhaa lakini zimechacha leo wakati ubalozi mpya wa Marekani umefunguliwa mjini Jerusalem hatua iliyowaghadhabisha Wapalestina. Wanaitazama hatua hiyo kama Marekani kuunga mkono utawala wa Israel katika mji huo mzima wakati wapalestina wanadai haki ya umiliki wa eneo la mashariki mwa mji huo. Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria. Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye. Israel ilichukua udhibi...

Tanzania yafungua ubalozi wake Israel, Mahiga aomba Israel ifungue ubalozi Dar es Salaam

Dkt Mahiga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel jijini Tel Aviv Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania. Afisi hizo za kibalozi zinapatikana katika mji wa Tel Aviv. Rais Magufuli mwezi Machi mwaka huu alikuwa amemualika Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi nchini Tanzania badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya. Waziri Mahiga, akizindua ubalozi huo Jumanne, alisema Watanzania hawataisahau Israel kwa kuwa ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ambalo mafanikio na mchango wa jeshi hilo unajulikana na kila Mtanzania. Alisema JKT baada ya lugha ya Kiswahili ndiyo chombo cha pili kilichosaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha makabila zaidi ya 120 ya Watanzania na kuwa wamoja ha...

Marekani yaishutumu Iran kuvuruga amani Mashariki ya Kati

Waziri mpya wa mamabo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameishutumu Iran kwa shughuli zake katika kanda ya Mashariki ya Kati, ambazo amesema zinaivurga kanda hiyo. Katika ziara  yake ya kwanza nje ya nchi  saa kadhaa baada ya kuapishwa Mike Pompeo alikutana na viongozi wa Saudi Arabia  na Israel nchi mbili ambazo zinamahusiano maalumu ya kimkakati na Marekani na ambazo pia zina adui wa pamoja Iran  huku waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu akisisitiza kuwa makubaliano ya nyukilia na Iran lazima yabadilishwe au yavunjwe ingawa mataifa mengi makubwa duniani  yanayaona makubaliano hayo kuwa ndiyo njia inayoweza kuizuia Iran isiwe na silaha za nyukilia. Akizungumza pembezoni mwa waziri mkuu wa Israel baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa masaa mawili mjini Telaviv  waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo  alisema nia ya Iran kutaka kutawala siasa za  Mashariki ya Kati bado ipo palepale na akasema hawatapuuza vitendo hivyo vya Iran k...

Palestina yazika wahanga, yailaani Marekani

MTEULE THE BEST Serikali ya Palestina imekataa wito wa Marekani kutaka sehemu ya Ukuta wa Magharibi katika Mji Mkongwe wa Jerusalem kubakia kwenye udhibiti wa Israel, huku maziko ya Wapalestina waliouawa kwenye maandamano wakizikwa Afisa wa ngazi za juu kwenye serikali ya Palestina, Nabil Abu Rudeineh, ameliambia shirika la habari la WAFA kwamba kamwe Wapalestina hawatakubali mabadiliko yoyote kwenye mpaka wa 1967 wa Jerusalem Mashariki. "Msimamo huu wa Marekani unathibitisha kwa mara nyengine kwamba utawala wa sasa wa nchi hiyo haupo kabisa kwenye suala la kupatikana amani na badala yake unataka kuuimarisha ukaliaji wa kimabavu," alisema. Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Marekani alisema kabla ya kuanza kwa ziara ya Makamu wa Rais Mike Pence kwenye mataifa ya Misri, Israel na Ujerumani, kwamba nchi hiyo haiwezi kuona "ni kwa namna gani Ukuta wa Magharibi usiwe sehemu ya Israel" hata ikiwa patakuwa na makubaliano baina ya Waisraeli na Wapalestina.  ...

Israel yaendeleza mashambulizi dhidi ya Hamas,kisa tangazo la Trump juu ya Jerusalem

Israel na Hamas waendeleza mapambano kis mji wa Jerusalem Jeshi la Israel limesema mashambulizi yake roket yanazilenga ngome tatu za kijeshi za wapiganaji wa kundi la Hamas,ikiwa ni hatua ya kujibu shambulizi dhidi yao la kutoka ukanda wa Gaza. Israel pia imeamuru kufungwa kwa mpaka kati yake na Gaza,baada ya shambulizi la nne maroketi yanayodaiwa kurushwa na kundi la HAMAS. Hali hii ya mapigano ya kundi la Hamas inadaiwa kuwa ni kutokana na hasira kufuatia hatua ya rais Trump kuutambua mji wa Jesrusalem kama makao makuu ya Israel. MATANGAZO Hata hivyo jeshi la Israel linasema kuwa makombora kati ya yaliyorushwa,walifanikiwa kuyazuia,ambapo moja lilianguka eneo la wazi kusini mwa Israel na jingine lilipoteza uelekeo

EU yajitenga na Netanyahu na Trump kuhusu Jerusalem

MTEULE THE BEST Netanyahu alikutana na Federica Mogherini mjini Brussels Mkuu wa sera ya mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya (EU) amepuuzilia mbali wito wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuutaka umoja huo uutambue mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Bi Federica Mogherini amesema mataifa wanachama wa umoja huo hawataitambua Jerusalem kabla ya mwafaka wa mwisho kati ya Israel na Wapalestina kutiwa saini. Amesema EU imeungana kwa pamoja kusisitiza kwamba Jerusalem inafaa kuwa mji mkuu wa Israel na pia taifa la Wapalestina litakapoundwa. Alikuwa akihutubu baada ya mkutano ambapo Bw Netanyahu alitoa wito kwa EU kuifuata Marekani katika kuitambua Jerusalem. Hatua ya Rais wa Marekani kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel imeshutumiwa vikali na Wapalestina na pia jamii ya kimataifa. Aidha, imeyakera sana mataifa ya Kiarabu na Kiislamu. Maandamano yameshuhudiwa katika maeneo ya Wapalestina Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, na pia katika balozi na Mare...