Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya POMBE

Walevi waunda kisiwa New Zealand kukwepa marufuku

MTEULE THE BEST Watu hao waliunda kisiwa kwa kutumia mchanga katika juhudi za kukwepa marufuku Wakazi kadha wa New Zealand walitumia ubunifu wa hali ya juu katika kinachoonekana kuwa juhudi za kukwepa marufuku ya kunywa pombe maeneo ya umma. Maji yalipokupwa baharini, walitumia mchanga kuunda 'kisiwa' kidogo katika sehemu ambayo mto Tairua unamwaga maji yake baharini katika rasi ya Coromandel Jumapili alasiri. Kisha, waliiweka meza yao ya safari na kufungua chupa zao za vinywaji na kuanza kujiburudisha. Wakazi walifanya mzaha kwamba walikuwa kwenye "eneo la bahari la kimataifa" lisilomilikiwa na taifa lolote hivyo hawangeathirika na marufuku hiyo ya pombe. Watu hao walibugia vinywaji vyao hadi usiku mkesha wa Mwaka Mpya na kutazama fataki zikirushwa kuukaribisha mwaka mpya kwa mujibu wa tovuti ya New Zealand ya stuff.co.nz. Kisiwa chao bado kilionekana Jumatatu asubuhi. Marufuku dhidi ya unywaji pombe hadharani ilitangazwa Coromandel kipindi cha mwaka mpya na ...