Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MITUMBA

BAKULI LA YANGA LAENDELEA ILI WAWEZE KUPATA NAULI YA KUPANDA NDEGE

Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City Jumapili hii hivyo kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amewaomba wanachama kuichangia timu ili iweze kufafiri kwa ndege na kiasi kitakachopelea yeye ataongezea. Kikosi cha Yanga Zahera ambaye hayupo nchini amedai kitendo cha timu kusafiri tarehe 27 na kwenda kucheza tarehe 29 sio rahisi kwenda kwa basi hivyo ni lazima iende kwa ndege ili iweze kupata matokeo. ''Mimi kocha Mwinyi Zahera naomba wanachama waichangie klabu iweze kusafiri kwa ndege kwenda Mbeya ili tukacheze na tupate matokeo na mimi binafsi nitaongezea kiasi kitakachopelea'', amesema Zahera. Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera Aidha Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo amesema matokeo ya Yanga ni muhimu kwa wanachama na timu nzima ili kuendelea kuongoza ligi kwahiyo kila mmoja anayo sababu ya kuhakikisha timu inasafiri vyema. Yanga kwasasa inaongoza ligi ikiwa na alama 47 kwenye ...

Rwanda hatarini kuadhibiwa na Marekani juu ya nguo za mitumba

Sera ya rais wa Marekani Donald Trump ya "Amerika Kwanza" kuhusu biashara ya kimataifa imeiathiri Rwanda, kwa kuanzisha ushuru wa nguo zinazotoka katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki . Ushuru huo unahusiana na suala zima la mitumba kutoka Marekani ambapo Rwanda imekataa kupokea nguo kuu kuu kutoka Marekani. Mzozo huu ulianza lini? Mnamo mwezi Machi 2018, Marekani iliipatia Rwanda muda wa siku 60 iwe imebadilisha msimamo huo, la sivyo itaondolewa uwezo iliyopewa wa nguo zake kwa Marekani bila ushuru - hadhi inayoipata chini ya makubaliano ya kibiashara baina ya Marekani na Afrika (Agoa). Agoa ni mpngo wa Marekani wa kibiashara wenye lengo la kuinua biashara na uwekezaji kwa mataifa yaliyotimiza vigezo vya kuondolewa ushuru wa bidhaa 6,500 zinazouzwa Marekani. "Nia ya rais inaonyesha azma yake ya kuhakikisha anatekeleza sheria zetu na kuhakikisha kunakua na usawa katika mahusiano yetu ya biashara ," alisema Naibu muwakilishi wa wafanya biashara ...