Sera ya rais wa Marekani Donald Trump ya "Amerika Kwanza" kuhusu biashara ya kimataifa imeiathiri Rwanda, kwa kuanzisha ushuru wa nguo zinazotoka katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki . Ushuru huo unahusiana na suala zima la mitumba kutoka Marekani ambapo Rwanda imekataa kupokea nguo kuu kuu kutoka Marekani.
Mzozo huu ulianza lini?
Mnamo mwezi Machi 2018, Marekani iliipatia Rwanda muda wa siku 60 iwe imebadilisha msimamo huo, la sivyo itaondolewa uwezo iliyopewa wa nguo zake kwa Marekani bila ushuru - hadhi inayoipata chini ya makubaliano ya kibiashara baina ya Marekani na Afrika (Agoa).
Agoa ni mpngo wa Marekani wa kibiashara wenye lengo la kuinua biashara na uwekezaji kwa mataifa yaliyotimiza vigezo vya kuondolewa ushuru wa bidhaa 6,500 zinazouzwa Marekani.
"Nia ya rais inaonyesha azma yake ya kuhakikisha anatekeleza sheria zetu na kuhakikisha kunakua na usawa katika mahusiano yetu ya biashara ," alisema Naibu muwakilishi wa wafanya biashara wa Marekani CJ Mahoney wakati huo.
Siku hizo 60 sasa zimekwisha.
Marais Donald Trump na Paul Kagame hawakuonekana kuwa karibu sana walipokutana mwezi Januari
Kwanini Rwanda ilipiga marufuku uagizwaji wa nguo kuu kuu?
Nia ni kulinda sekta yake changa ya viwanda vya nguo.
mengi miongoni mwa mataifa ya Afrika wakati mmoja yaliwahi kuwa na sekta zinazofanya vema za viwanda vya nguo. Lakini baada ya miongo kadhaa ya utawala mbaya na ukosefu wa amani na utulivuna ushindani duniani sekta hiyo ilidolola.
Hali hii inaweza kuonekana nchini Ghana, ambako utafiti ulibaini kuwa wakati sekta ya viwanda vya nguo ilipo binafsishwa miaka ya 1980 kulishuhudiwa kusshuka kwa ajira kwenye viwanda vya nguo na uzalishaji wa nguo kwa ujumla - kutoka watu 25,000 mwaka 1977 hadi watu 5,000 mwaka 2000.
Kenya ilikuwa na wafanyakazi laki tano wanaofanya kazi kwenye viwanda vya nguo .
Takriban asilimia 67% ya watu katika Mataifa ya Afrika Mashariki hununua baadhi ya nguo zao kwenye masoko ya mitumba , ulibaini uchunguzi wa shirika la Misaada ya kimataifa la Marekani USAID.
Masoko ya nguo za mitumba kama hili la Gikomba jijini Nairobi hupatikana kote barani Afrika
Serikali za Afika Mashariki zinadai kuwa viwanda vya ndani ya nchi zao vinaathiriwa na nguo za mitumba.
Kwa hiyo mwaka 2015, mataifa ya Afrika Mshariki yalitangaza kwamba nguo za mitumba zitapigwa marufuku kwenye masoko ya nchi hizo kuanzia 2019.
Nchini Rwanda, serikali ilisema kuwa uvaaji wa nguo za mitumba unatishia hadhi ya watu wake
Rwanda iliongeza ushuru wa nguo za mitumba zinazoagizwa nje kutoka $0.20 hadi dola $2.50 kwa kilo moja ya nguo hizo mwaka 2016.
Lengo ni kumaliza kabisa matumizi ya nguo za mitumba.
Ni matumaini ya serikali kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza na kuboresha sekta ya viwanda vya nguo na kubuni ajira kwa watu zaidi ya 25,000.
Kupotea kwa mitumba kumewaathiri wanyaruanda?
Uhaba wa nguo za mitumba kikwazo kwa wanyaruanda
Rulinda Elmass ambaye ni mfanyabiashara wa mitumba anasema mwanzoni mwa uamuzi huu,nguo za mitumba zilikuwa tunazipata kwa bei kubwa,lakini sasa hamna hata kidogo.
"athari ni nyingi,duka langu lilikuwa limejaa nguo lakini sasa hamna kitu,nitafunga milango, walikuepo walanguzi wakubwa wa mitumba lakini wao walihamishia biashara zao nchini Congo."
Aidha mfanyabiashara huyo aliongeza kwa kudai kwamba hali ya maisha ndio inafanya zoezi hili kuwa gumu zaidi na kama vikwazo vya Marekani vitakuepi basi tatizo litaongezeka kuwa kubwa zaidi."
''siyo kwamba tunakataa mpango wa serikali kuimarisha viwanda vya nguo,lakini bado ni vichache na ingekuwa vizuri wakubali ushindani wa viwanda wanavyotaka na nguo za mitumba ,kila mtu akanunua anachotaka"
Kama Marekani wakiweka vikwazo nchini Rwanda,athari zitaongezeka
''Ni tatizo kubwa kupata nguo sokoni, zamani mtu alikuwa na franga elfu 10 na kuweza kupata nguo safi za mitumba na tena aina tofauti,shati na suruali kadhaa,lakini sasa ni nguo kutoka China ambazo bei yake iko juu sana,shati moja franga elfu 10 hadi 15 siyo rahisi kuinunua.Ni kweli Rwanda inataka kuendeleza viwanda vyake ndiyo maana wanasema made in Rwanda lakini hatujaziona na kama hawajaanza kuzitengeneza basi waweza kuachia nguo za mitumba kidogo ambazo zinatufaa sisi ambao uwezo wetu ni mdogo''anaeleza Florean ambaye ni mteja wa nguo hizo.
Image captionZamani alikuwa anafanya kazi mpaka jioni lakini sasa anafanya kazi mpaka saa sita na anasema kupata mitumba ni gharama kubwa sana na sio mizuri
Kwa nini Marekani imekasirika?
Tatizo lenyewe lilianza wakati shirika la biashara nchini Marekani ilipowasilisha malalamiko yake kwa Shirika la Wawakilishi wa Wafanyabiashara la Marekani (USTR), wakisema kuwa uamuzi wa mataifa ya Afrika Mashariki wa kuondosha mitumba ya Marekani kwenye masoko yao unasababisha hali ngumu ya kiuchumi.
Inakadiriwa kuwa marufuku ya mauzo ya mitumba kwenye masoko ya Afrika Mashariki kunaweza kusababisha watu 40,000 kukosa kazi nchini Marekani na mauzo ya nje ya dola milioni 124.
Kwa nini Kenya, Uganda na Tanzania zinaunga mkono biashara ya mitumba?
Tisho kutoka kwa Marekani lilikuwa kubwa kuwafanya waachane na mpango wao wa kupiga marufuku mitumba
Kati kati mwa mwaka 2017, Kenya ilisema itaheshimu makubaliano ya Agoa na aikamua kuondoa mapendekezo yake ya ku kupiga marufuku nguo hizo.
Faida ya Kenya kutoka Agoa ni kubwa kuliko ambayo Rwanda inaipata. Mauzo yake kwa Marekani yalifikia karibu dola milioni 600 mwaka 2017, ikilinganishwa na Rwanda ambayo iliuza takriban bidhaa za dola Milioni 43 tu.
Rwanda imeazimia kuwa taifa lenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2020
Inachokifanya Marekani ni haki?
Ndio na hapana. marekaniina kila haki chini ya mkataba wa Agoa wa kuzitaka nchi kuondoa vikwazo vya kibiashara vilivyoainishwa katika mkataba huo.
"Lakini hilo halimaanishi inachokifanya ni cha haki ," alisema Bw Mr Harris. "Lengo kuu la Agoa ni kutumia biashara kusaidia maendelei na ukuaji wa kiuchumi ."
Aliongeza kuwa Marekani huondolea usuru wa forodha mataifa mengi mengine kwneye soko lake ambayo yameweka vikwazo kwa mauzo ya Mrekani kama vile India na Brazil. " Kama Marekani inataka kuchukua msimamo na kuchukua hatua kwa kila nchi, itakua ni kuzuwia bidhaa zake jamnbo ambalo litakuwa la maana zaidi.
Sekta ya nguo za mitumba nchini Rwanda ina thamani ya karibu dola milioni 20
Rais wa Rwanda Paul Kagame anaonekana kuwa Rwanda Paul Kagame anaonekana kujitolea kwa ajili ya ukuaji wa uchumi.
"Hili ni chaguo tulilooina kuwa hatuna budi kulichagua. Kulingana na ninavyoona kuchagua ni rahisi , licha ya kwambatunaweza kupata athari zake," alisema Kagame mwaka 2017.
"Rwanda na mataifa mengine ya kikanda ambayo ni mwanachama wa Agoa, wanapaswa kufanya mambo mengine - tunapaswa kukua na kuanzisha viwanda vyetu."
Mshindi halisi katika mgogoro huu atakuwa ni Uchina, anasema mtaalam. mauzo ya bidhaa nafuu, na nguo mpya kwa mataifa ya Afrika Mashariki ni y thamani ya dola bilioni $1.2 bn, kulingana na USAID survey
Maoni