Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wanaotaka kustaafu wapewa onyo


Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Bi. Winifrida Rutahindurwa amewaonya waalimu wanaofanya udanganyifu katika taarifa zao za kiutumishi kwa lengo la kujiongezea muda wa kuwepo katika utumishi wa umma licha ya kuwa umri wao wa kustaafu kwa mujibu wa sheria kufika.




Bi. Rutahindurwa ametoa kauli hiyo Mei 29, 2018 mjini Bagamoyo alipokutana na waalimu wakuu na wakuu wa shule za umma kutoka wilaya za Bagamoyo na Chalinze kwa lengo la kutoa elimu juu ya wajibu wao na kusema kuwa  kuna wakati walimu walitakiwa kupeleka taarifa zao za kiutumishi kwa waajiri wao lakini baadhi yao walipeleka taarifa tofauti na zile walizojaza kwenye mikataba ya kazi wakati wa kuanza ajira.

"Kuna baadhi ya waalimu wanajifanya hawakumbuki walizaliwa mwaka gani wakati walijaza mikataba wakati wanaanza ajira na wengi wao wamebadilisha taarifa zao na kujipunguzia umri jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria", amesema Bi. Rutahindurwa.

Aidha, Bi. Rutahindurwa amefafanua kuwa mwalimu atakapoandikiwa kibali cha kustaafu, TSC pamoja na mfuko wamifuko ya hifadhi ya jamii wanajikita zaidi kuangalia taarifa za mwalimu alizojaza awali wakati anaanza ajira yake na sio kutegemea taarifa za stakabadhi ya mishahara peke yake.

"Naomba muwaeleze walimu wote katika shule zenu kuwa utakapoandikiwa kibali cha kustaafu sisi tunaangalia zaidi taarifa zako ulizojaza wakati unaajiriwa na ukibainika umedanganya utachukuliwa hatua kwa kuwa umemwibia mwajiri", amesisitiza Bi. Rutahindurwa.

Kwa upande wao waalimu walionesha kupokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuondoa usumbufu kwa mwalimu pale anafuatilia masuala yake ya mafao mara baada ya kustaafu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...