Maelfu ya mashabiki wa miamba wa Uhispania Real Madrid walijitokeza katika barabara za jiji kuu la Uhispania Madrid kuwapokea wachezaji wa klabu hiyo waliporejea kutoka Kiev Jumapili.
Madrid walishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya tatu mtawalia baada ya kuwalaza Liverpool ya Uingereza 3-1 katika mechi iliyokumbwa na utata kutokana na kuumizwa kwa nyota ya Misri anayechezea Misri Mohamed Salah.
Fainali hiyo ilitawaliwa na machozi, makosa na bao la kipekee kutoka kwa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale.
Jumapili jijini Madrid, mashabiki wa Real walishangilia na kupeperusha hewani skavu zenye rangi na nembo za klabu hiyo na ujumbe wa kuisifu klabu hiyo basi la wazi lililokuwa limewabeba wachezaji na wakuu wa timu hiyo wakiwa na kikombe lilipopitia barabara za jiji hadi uwanja wa kawaida wa kusherehekea, uwanja wa Plaza de Cibeles.
Basi hilo kubwa la rangi nyeupe lilikuwa limeandikwa 'Campeones 13' na kuchorwa nembo ya klabu, kuashiria ushindi mara 13 wa ubingwa Ulaya.
Nahodha Sergio Ramos (kulia) na Marcelo waliongoza sherehe Madrid
Maelfu ya mashabiki waliilaki timu hiyo iliporejea Madrid Jumapili
Mashabiki walikusanyika katika uwanja wa Cibele, Madrid kusherehekea
Nahodha Sergio Ramos alishuka na kikombe kutoka kwenye ndege klabu hiyo iliporejea Madrid Jumapili
Kwingineko, ilikuwa masikitiko kwa Mohamed Salah na wachezaji wenzake wa Liverpool waliporejea nyumbani uwnaja wa ndege wa John Lennon ...
kwa mashabiki wa Liverpool ilikuwa vile vile, huzuni na masikitiko
Maoni