Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya IKULU

Rais Samia amefungua Mkutano wa 14 wa Baraza la Biashara (TNBC)

  Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo June 09,2023 amefungua na kushiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Biashara (TNBC), Ikulu Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba kazi kubwa inaendelea kufanyika ya kuboresha mifumo ya TEHAMA kwenye Sekta za Umma ili ianze kusomana ambapo ameahidi kuwa sio zaidi ya miezi sita RAISkinachotokea Bandarini atakuwa anaweza kukisoma akiwa Ikulu. Rais za Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Juni, 2023. Rais Samia amenukuliwa akisema “Kazi kubwa inaendelea kufanyika ya kuboresha mifumo ya TEHAMA, mifumo yetu haisomani, taarifa hazioani, kazi tunayokwenda kufanya kwa nguvu kubwa sasa ni kufanya mifumo ndani ya Sekta ya Umma isomane pia iwe na vigezo vya Kimataifa” “Changamoto zilizotajwa hapa hizo za Kariakoo na nini ni kwamba mifumo yetu haijaweza kuchukua taarifa zote hizo, kazi iliyopo sasa ni...

Museveni: siwezikuachia kiti cha urasi

Museveni aweka wazi mipango ya kutoachia madaraka Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amewaambia wazi wapinzani wake kuwa hana mpango wa kuachia madaraka hivi karibuni, hivyo waachane na mawazo yao ya kuwaza kiti hicho. Rais Museveni ameyasema hayo kwenye mkutano wa ndani wa chama ambao uliwakusanya pamoja viongozi wa vyama vilivyopo Bungeni, mkutano uliofanyika Jijini Kampala. Museveni amesema amefurahia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo, ambapo aliwaambia wapinzani wake kwamba hatofikiria kubadilishana madaraka mpaka pale atakaporidhishwa na Ustawi na usalama wa kimkakati wa nchi za Afrika. “Nasikia watu kama Mao wanazungumzia kuachia madaraka, ni kwa namna gani watakaa kwenye umati na kumuona Museveni akikabidhi madaraka. Hicho ndicho kitu muhimu kwake. Sidhani kama ni sahihi kwa yeye kusema hivyo, badala ya kuzungumzia hatma ya Afrika, mnaongelea vitu visivyo na maana, uchaguzi, nani atakuwa nani. Na ndio kwa sababu nilisema kama bado nina ...

Makamu wa Rais akutana na Mabalozi wa Palestina na Japan Ikulu

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amekutana na Balozi wa Palestina pamoja na Balozi wa Japan jijini Dar es salaam.    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Mansour AbuAli (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Shinichi Goto (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha, Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Magufuli afanya uteuzi tume ya madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Manya umeanza leo tarehe 01 Juni, 2018. Kabla ya uteuzi huo Prof. Manya alikuwa Kamishna wa Madini na alikuwa akikaimu nafasi ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. David Mulabwa kuwa Kamishna wa Madini. Kwa habari kamili soma hapa chini...