Rais Trump ameyatusi mataifa ya Afrika , haiti na El salvador akidai ni machafu Rais wa Marekani amewashutumu wahamiaji wanaoingia nchini humo kwa kuwatusi katika afisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse. ''Kwa nini tunawaruhusu watu hawa kutoka mataifa 'machafu''?. Rais Trump aliwaambia wabunge siku ya Alhamisi kulingana na gazeti la The Washington Post. Tamko hilo lilidaiwa kuwalenga watu kutoka Afrika, Haiti na El Salvador. Ikulu ya Whitehouse haikukana tamko hilo ambalo lilithibitishwa na vyombo vyengine vya habari. ''Wanasiasa fulani wa Washington hupendelea kupigania mataifa ya kigeni, lakini rais Trump atawapigania raia wa M arekani pekee,taarifa iliotoka katika msemaji wa Ikulu Raj Sha ilisema. Iliendelea: Kama mataifa mengine ambayo yana wahamiaji wanaofaa kuwa nchini humo, rais Trump anapigania suluhu ya kudumu inazofanya taifa hilo kuwa thabiti kwa kuwakaribisha wale ambao wana mchango katika jamii ,hukuza uchumi wetu ...