Alexis Sanchez
Manchester City wameipatia Arsenal dau la Ā£20m ili kumsajili Alexis Sanchez, 29, huku mshambuliaji huyo wa Chile akidaiwa kukubali malipo ya Ā£250,00 kwa wiki..(Guardian)
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anatarajiwa kuilipa Boca Juniors kitita cha pauni milioni 27 kumsajili Cristian Pavonkatikaligi Premia. (TyC Sports - in Spanish)
Wakati huohuo, Wenger anatarajiwa kukaa katika viti vya mashabiki katika uwanja wa Stamford Bridge kwa mechi ya Jumatano ya nusu fainali ya kombe la carabao baada ya kupigwas marufuku ya kukaa katika eneo la wakufunzi (Express)
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hataki kuwasajili wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho licha ya kuwa nyuma ya viongozi wa ligi ya La Liga Barcelona.. (Reuters)
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic huenda akaondoka Old Trafford kabla ya kukamilika kwa msimu huu.
Raia huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 36 hana kandarasi na klabu hiyo. (Yahoo Sport)
Everton imetoa chanagamoto kwa Southampton katika ushindani wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 28, kwa Ā£20m. (Mail)
Liverpool na Arsenal watalazimika kulipa takriban Ā£90m kumsajiuli mshambuliaji wa Monaco Thomas Lemar, 22. (Mirror)
lakini kulingana na mwandishi wa Ufaransa Julien Laurens, huenda akachelewesha uhamisho wake Liverpool kutokana na michuano ya kombe la dunia (5 live's Euro Leagues podcast)
Winga wa Brazil Lucas Moura, 25, amekubali kujiunga na manchester United kutoka Paris St-Germain, ijapakuwa kitita cha uhamisho huo hakijakubalika kati ya vilabu hivyo viwili. (Gazetta dello Sport - in Italian)
Arsenal itawasilisha rasmi ombi jipya la kandarsi mpya ya kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuanza mazungumzo na Arsenal katika kipindi cha wiki moja ijayo na atalazimika kupunguza mshahara wake ili kusalia klabu hiyo. (Mirror
Maoni