Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wachezaji wa thamani ya juu zaidi duniani watajwa


Harry Kane alifunga mabao 56 mwaka jana akichezea klabu na taifa


Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ameorodheshwa kuwa wa tatu miongoni mwa wachezaji wa thamani ya juu zaidi duniani, kwa mujibu wa utafiti mpya.


Utafiti huo wa shirika la takwimu za michezo la CIES unasema Kane thamani yake ni euro 194.7m (Ā£172.65m).


Wanaomzidi ni mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 25, na mwenzake wa Barcelona Lionel Messi, 30, pekee.


Mshambuliaji huyo wa England mwenye miaka 24, alifungia klabu na taifa mabao 56 mwaka jana, na kumfanya mfungaji mabao bora zaidi Ulaya.


Mwenzake wa Spurs na England Dele Alli, 21, yumo nafasi ya sita oordha hiyo na ndiye wa pili orodha hiyo kwa wachezaji walio Ligi ya Premia.


CIES walitumia umri, nafasi anayocheza mchezaji, muda wa mkataba wake, uchezaji wake uwanjani na hadhi yake kimataifa kufanya makadirio hayo ya thamani.


Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26, fowadi wa Manchester United Romelu Lukaku na kiungo wa kati Paul Pogba, wote wa miaka 24, ndio wachezaji wengine wanaocheza England walio kwenye 10 bora.


Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, aliyetawazwa mchezaji bora zaidi wa kiume duniani na Fifa 2017 yumo nafasi ya 49 kwenye orodha hiyo.


Thamani yake ni euro 80.4m (Ā£71.29m)


Mchezaji mpya wa Barcelona Philippe Coutinho, 25, amewekwa nafasi ya 16 ,thamani yake ikikadiriwa kuwa Ā£33m chini ya bei ambayo Barca walilipa Liverpool kumchukua.


Kipa wa thamani ya juu zaidi ni Marc-Andre ter Stegen, 25, wa Barcelona ambaye thamani yake ni euro 96m (Ā£85.13m) na Samuel Umtiti, 24, ndiye beki ghali zaidi, thamani yake ikiwa euro 101m (Ā£89.56m).


Paulo Dybala, 24, wa Juventus ndiye wa thamani ya juu zaidi Serie A thamani yake ikiwa Ā£155.18m naye Robert Lewandowski, 29, wa Bayern Munich anaongoza kwa wachezaji wa Bundesliga (Ā£94.88m).


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...