Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 11.01.2018


Winga wa Arsenal Theo Walcot


Everton imejiunga na vilabu vilivyo na hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot 28.


Muingereza huyo pia anasakwa na klabu yake ya zamani Southampton huku Arsenal ikidaiwa kutaka dau la Ā£30m. (Liverpool Echo)


Mchezaji wa RB Leipzig na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita huenda akajiunga na Liverpool mwezi huu.


Mchezaji wa RB Leipzig na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita huenda akajiunga na Liverpool mwezi huu.


Liverpool tayari wamemsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa dau la Ā£48m lakini wanaweza kulipa kati ya Yuro milioni 15-20 ili kumchukua kabisa.(Bild - in German)


Mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Kaskazini Martin O'Neill


Mkufunzi wa Jamhuri ya Ireland Kaskazini Martin O'Neill alitarajiwa kukutana na maafisa wa klabu ya Stoke siku ya Jumatano kuhusiana na wadhfa wa mkufunzi ulio wazi huku naibu wake Roy Keane pia akitarajiwa kuondoka iwapo atachukua wadhfa huo. (Irish Independent)


Guangzhou Evergrande wanasema kuwa hawatashindana na klabu pinzani ya ligi ya Super Beijing Guoan kupata hudumu za mchezaji wa Gabon na Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang (ESPN)


Dele Alli ni kiungo wa kati wa klabu ya Tottenham


Tottenham imeanza mazungumzo yasio rasmi na kiungo wa kati Dele Alli. Klabu hiyo inadaiwa kuwa na matumaini ya kutia saini kandarasi mpya na mchezaji huyo wa Uingereza. (Daily Mirror)


Naibu mwenyekiti wa klabu ya Fullham Tony Khan amesema kuwa beki wa kushoto wa klabu hiyo Ryan Sessegnon, 17, hatauzwa licha ya kusakwa na Manchester United na Tottenham Hotspurs. (Daily Telegraph)


Manchester United italazimika kulipa hadi Ā£27m ili kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Leander Dendoncker kutoka Anderlecht mnamo mwezi Januari.(Manchester Evening News)


Mshambuliaji wa West ham na Senegal Diafra Sakho


Crystal Palace huenda ikakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Senegal Diafra Sakho, 28, kutoka West Ham mwishoni mwa wiki . (Daily Mirror)


Huddersfield imekubali kuingia mkataba na winga wa Norwich Alex Pritchard, 24. Raia huyo wa Uingereza aliondoka Tottenham kwa dau la Ā£8m katika dirisha la uhamisho la 2016. (Daily Mail)


West Ham wameambiwa watalazimika kulipa Ā£15m ili kumsajili kiungo wa kati wa Bournemouth na Republic of Ireland Harry Arter, 28. (Daily Mirror)


Kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos ameambia klabu hiyo kwamba anataka kuondoka


Kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos ameambia klabu hiyo kwamba anataka kuondoka huku Liverpool ikidaiwa kuwa na hamu ya kumsajili raia huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 21. (Diario Gol - in Spanish)


Hearts wanajiandaa kumsajili beki wa kushoto wa Manchester United Demetri Mitchell kwa mkopo.


Beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20 atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu hiyo ya Uskochi wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari.(Edinburgh Evening News)


Beki wa Barcelona Gerard Pique ameionya Manchester United kwamba beki mwenza Samuel Umtiti atasalia katika klabu hiyo kwa ''miaka mingi ijayo''


Beki wa Barcelona Gerard Pique ameionya Manchester United kwamba beki mwenza Samuel Umtiti atasalia katika klabu hiyo kwa ''miaka mingi ijayo'' .


Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 anaweza kuondoka katika klabu hiyo baada ya Barcelona kulipa kitita cha kumwachilia cha Ā£55m mbali na dau la uhamisho huo(Metro)


Wakati huohuo klabu hiyo ya Catalan inakaribia kumsajili beki wa Palmeiras Yerry Mina. Raia huyo wa Colombia ataweka saini ya kandarasi ya miaka mitano na nusu . (Radio Catalunya - in Spanish)


Javier Mascherano


Anatarajiwa kuchukua mahala pake beki wa Barca na Argentina ,33, Javier Mascherano ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu ya ligi ya Superleague nchini China Hebei China Fortune. (Goal)


Kiungo wa kati wa Ujerumani na Juventus Sami Khedira, 30, anasema kuwa hayuko tayari kucheza nchini Marekani na anataka kusalia mjini Turin wakati ambapo kandarasi yake itakamilika 2019(Gazzetta dello Sport)


Millwall imewasiliana na Aston Villa kuhusu kumsajili beki mwenye umri wa miaka 30 Tommy Elphick kwa mkopo kwa kipindi cha msimu kilichosalia.


Sami Khedira


Meneja wa Villa Steve Bruce amekataa kuondoa uwezekano wa mchezaji huyo kuondoka klabu hiyo mwezi huu. (Birmingham Mail)


Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anatarajiwa kusisitiza ombi lake kwa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley na mkurugenzi mkuu Lee Charnley kuhakikisha kuwa wachezaji wanasaini kandarasi mpya kabla ya kukamilika kwa muda wa mwisho aliouweka wa tarehe 20 Januari. (Newcastle Chronicle


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...