Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya RONALD

Ronaldo amchana Messi, amtaka abadilike

Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo ameibuka na kumzungumzia nyota wa Barcelona, Lionel Messi akisema angependa kumuona mchezaji huyo akicheza katika ligi kuu nchini Italia 'Serie A'. Cristiano Ronaldo na Lionel Messi Cristiano Ronaldo amemhimiza mpinzani wake huyo wa muda mrefu Lionel Messi, akimtaka  "kukubali changamoto" na kumfuata nchini Italia. Alipoulizwa kama anamuhitaji Messi au la!, Ronaldo amesema, " hapana, labda yeye ndiyo ananihitaji mimi. Nimecheza Ureno, Uingereza, Hispania, Italia na kwenye timu ya taifa pia, lakini yeye bado yuko kwenye timu moja. Labda yeye kama ananihitaji mimi ". " Kwangu mimi maisha ni changamoto, ninapenda hivyo na ninapenda kuwafanya watu wangu wawe na furaha. Ningependa siku moja nayeye aje kucheza Italia kama nilivyofanya mimi, akubali changamoto, lakini kama ana furaha pale alipo ninaheshimu uamuzi wake ", ameongeza Ronaldo. Aidha Cristiano amemzungumzia Messi kama ni mchezaji mkubwa...

Kwa Picha: Real Madrid walivyosherehekea kulaza Liverpool na kushinda Champions League

Maelfu ya mashabiki wa miamba wa Uhispania Real Madrid walijitokeza katika barabara za jiji kuu la Uhispania Madrid kuwapokea wachezaji wa klabu hiyo waliporejea kutoka Kiev Jumapili. Madrid walishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya tatu mtawalia baada ya kuwalaza Liverpool ya Uingereza 3-1 katika mechi iliyokumbwa na utata kutokana na kuumizwa kwa nyota ya Misri anayechezea Misri Mohamed Salah. Fainali hiyo ilitawaliwa na machozi, makosa na bao la kipekee kutoka kwa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale. Jumapili jijini Madrid, mashabiki wa Real walishangilia na kupeperusha hewani skavu zenye rangi na nembo za klabu hiyo na ujumbe wa kuisifu klabu hiyo basi la wazi lililokuwa limewabeba wachezaji na wakuu wa timu hiyo wakiwa na kikombe lilipopitia barabara za jiji hadi uwanja wa kawaida wa kusherehekea, uwanja wa Plaza de Cibeles. Basi hilo kubwa la rangi nyeupe lilikuwa limeandikwa 'Campeones 13' na kuchorwa nembo ya klabu, kuashiria ushindi mara 13 wa ub...

Sababu ya Ronaldo kuorodheshwa wa 49 duniani

Ronaldo, atakuwa na miaka 33 mwaka huu, na alitawazwa mchezaji bora duniani miaka 4 kati ya tano iliyopita Cristiano Ronaldo amefunga mabao 58 miaka miwili iliyopita na kuwasaidia Real Madrid kushinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili mtawalia na pia La Liga mara moja. Miaka hiyo miwili iliyopita, ameshinda tuzo ya mchezaji bora duniani, tuzo ya Ballon D'Or, mtawalia. Anafaa basi kuwa mchezaji bora zaidi duniani na thamani yake kuwa ya juu zaidi? Ni kweli uchezaji wake hauna kifani. Lakini kwa thamani, la hasha. Utafiti huo wa shirika la takwimu za michezo la CIES Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la takwimu za michezo la CIES iliyotolewa Jumatano, mchezaji huyo ni wa 49 kwa thamani duniani. Anayeongoza orodha hiyo ni mshambuliaji wa Paris St-Germain ya Ufaransa, Mbrazil Neymar, 25, ambaye ndiye mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi na klabu yoyote duniani na mwenzake wa Barcelona Lionel Messi, 30, kutoka Argentina. Mshambuliaji wa To...