Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CUBA VS MAREKANI

Je Fidel Castro alikuwa mtu wa aina gani?

Fidel Castro aliitawala Cuba kama taifa lenye mfumo wa chama kimoja kwa takriban nusu karne Tawala za kijamaa zilianguka kote duniani , lakini Castro aliendelea kupeperusha bendera nyekundu karibu na maadui wake wakubwa, Marekani. Kiongozi huyo mwenye utata alisifiwa na wafuasi wake kama kiongozi wa ujamaa, askari mwanasiasa ambaye aliirejesha Cuba mikononi mwa watu. Lakini alikabiliwa na shutuma kwa kuwazima wapinzani wake kwa njia ya mateso na kwa kuwa na sera ambazo ziliporomosha uchumi wa Cuba. Fidel Alejandro Castro Ruz alizaliwa tarehe 13 Agosti 1926, nje ya ndoa ya familia ya mkulima bwanyenye , Angel María Bautista Castro y Argiz, ammbaye alihamia Cuba kutoka Uhispania. Mama yake , Lina Ruz González alikuwa kijakazi aliyefanya shughuli za shamba ambaye baadae alikuwa mpenzi wa baba yake ,na baadae ,baada ya kuzaliwa kwa Fidel, akawa mkewe. US LIBRARY OF CONGRESSImage captionBatista (Kushoto) aliungwa mkono na Marekani Castro alisoma katika shule ya kikatol...

Cuba yakana kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani

MTEULE THE BEST Cuba yakana kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani Cuba inasema kuwa hakujakuwa na mashambulizi ya kutumia sauti dhidi ya wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani kwenye mji wake mkuu Havana, ikisema kuwa madai hayo ni kisiasa yenye lengo la kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Cuba Bruno Rodriguez alipinga madai hayo ya kuwepo mashambulizi ya sauti akiyataja kuwa kuwa uwongo. Marekani yatathmini kufunga ubalozi wake Cuba Marekani inasema kuwa karibu wafanyakazi wake 20 katika ubalozi wake walikumbwa na matatizo ya kiafya na kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na kisa hicho. Ripot zinasena kwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na mashambulizi ya sauti lakini hata hivo hakuna kile kimethibitishwa. Marekani haijailaumu Cuba kwa mashambulizi hayo, na serikali ya Cuba imekana mara kwa mara kuwalenga wafanyakazi wa ubalozi. wa Marekania mjini Cuba. Marekani iliwatimua wanadiplomasia watano wa Cuba, ikis...