Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAANDAMANO

Polisi wa Kenya Wapiga Marufuku maandamano ya Upinzani

Polisi nchini Kenya wamepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumatatu jijini Nairobi.  Maandamano yaliyopendekezwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ni kinyume cha sheria, kulingana na Inspekta Mkuu wa Polisi Japhet Koome.  Kile ambacho serikali iliita maandamano yasiyoidhinishwa katika miji kadhaa ya Kenya Jumatatu iliyopita yaligeuka kuwa ghasia, na kuua mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu na kujeruhi wengine kadhaa.  Waandamanaji waliwarushia mawe polisi wa kutuliza ghasia nje ya ofisi za serikali katika mji mkuu na kuchoma matairi barabarani.  Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na kuwakamata viongozi watatu wa upinzani na zaidi ya waandamanaji 200.

Silaha kwa Wafaransa Waasi? Moscow Yapendekeza Mbinu ya Macron Kukabiliana na Ghasia Zinazoendelea.

​ Silaha kwa Wafaransa Waasi? Moscow Yapendekeza Mbinu ya Macron Kukabiliana na Ghasia Zinazoendelea. Zaidi ya watu milioni moja wameripotiwa kujiunga na maandamano kote Ufaransa siku ya Alhamisi dhidi ya mipango ya mageuzi ya pensheni ya Rais Emmanuel Macron, huku watu 80 wakikamatwa na ghasia zikiendelea hadi Mfalme Charles akakatiza ziara yake ya siku tatu.  Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilimpa Rais wa Ufaransa anayekabiliwa na mzozo suluhisho la ulimi-kwa-shavu kulingana na madai ya Paris ya demokrasia nchini Ukraine.  "Na ni lini Macron ataanza kuwasilisha silaha kwa raia wa Ufaransa ili kulinda demokrasia na uhuru wa nchi?" Msemaji wa FM Maria Zakharova aliandika kwenye chaneli yake ya Telegram. 

Maandamano ya kumuunga mkono Morales

Mamia ya waandamanaji walikusanyika katika ubalozi wa Bolivia nchini Argentina wakimuunga mkono Evo Morales Mamia ya watu nchini  Argentina  wameandamana kuonyesha kumuunga mkono  Evo Morales   Rais wa  Bolivia  aliyelazimisha na jeshi la nchi hiyo kujiuzulu. Raia wa Bolivia wanaoishi nchini Argentina kwa uratibu wa asasi za kiraia zenye mrengo wa kushoto walikusanyika mbele ya ubalozi wa Bolivia nchini Argentina. Waandamanaji hao walilaani hila alizofanyiwa Rais Morales katika uchaguzi na baada ya uchaguzi na kutolea wito jamii la kimataifa kumuunga mkono Morales. Waandamanaji hao walibeba mabongo yenye ujumbe kama “Hatutaki mapinduzi Bolivia” pia walikuwa wakipeperusha bendera yenye rangi 7 inayowakilisha wakazi wa  eneo la milima ya Andes pamoja na bendera za Bolivia.

Kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Awad Ibn Auf kwanini amejiuzulu

Bwana Ibn Auf ameondoka madarakani siku moja baada ya kuwa mkuu wa baraza la jesi Mkuu wa baraza la Jeshi la Sudani amejiuzulu siku moja baaba ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir yaliyosababishwa na wimbi la maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. Waziri wa ulinz Awad Ibn Auf alitangaza uamuzi huo kwenye TV, na kumtaja mrithi wake Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan. jeshi limesema kuwa litaendelea kuwa madarakani kw amiaka miwili na baadae utafanyika uchaguzi. Lakini viongozi wa maandamano wanasema hawataondoka mitaani hadi jeshi litakapokabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia. Kuanguka kwa Bwana Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza mwezi Disemba mwaka jana ambapo waandamanaji walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu. Bwana Ibn Auf alikuw amkuu wa ujasusi katika jeshi wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007. James Copnal...

Maandamano Sudan: Vikosi vya jeshi vyazozana Khartoum

Baadhi ya wanajeshi wameanza kuwalinda waaandamanaji mjini Lkhartoum baada ya vikosi vya usalama kurusha vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji kulingana na mashahidi. Wanajeshi walionekana wakijaribu kuyafukuza magari yaliokuwa yakijaribu kurusha vitoa machozi katika siku ya pili ya maandamano ya kutaka rais Omar al-Bashir kung'atuka uongozini. Waandamanaji walionekana wakitafuta hifadhi katika kifaa cha jeshi la wanamaji huku wasiwasi kati ya majeshi ukioonekana wazi. Bashir kufikia sasa amekataa kuondoka mamlakani ili kutoa fursa kwa serikali ya mpito. Maelfu ya waandamanaji wamekita kambi nje ya makao makuu ya jeshi nchini Sudan, wakimtaka rais Omar al-Bashir ajiuzulu. Inavyoonekana wanatarajia mapinduzi ya ndani ya nchi, wakiliomba jeshi kumtimua Bashir na kufungua njia ya kupatikana serikali ya mpito. Ni maandamano makubwa dhidi ya Bashir tangu kuzuka ghasia mnamo Desemba mwaka jana. Bashir amekataa kuondoka, akieleza kwamba wapinzani wake wanastahili kutafuta u...

RPC Gilles Muroto: Watakaoandamana Dodoma watapigwa hadi kuchakaa

Raia watakaondamana kwa lengo la kuwashinikiza wabunge kushirikiana na Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG nchini Tanzania watakiona cha mtema kuni. Onyo hilo limetoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ambaye amewatahadharisha waliopanga maandamano hayo hapo siku ya Jumanne kwamba watapigwa hadi ''kuchakaa''. Afisa huyo amesema kwamba baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo ACT Wazalendo wamepanga kufanya maandamano kesho kulishinikiza Bunge kufuta kauli yake ya kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad. Muroto ameonya kuwa wale wanaopanaga kufanya safari kuelekea mjini Dodoma ili kushiriki katika maandamano hayo wataambulia kupigwa na kuchakaa. ''Wale wote waliopanga kufanya maandamano mnamo Aprili 9, 2019 wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa," amesema Muroto. Afisa huyo amesisitiza kuwa maswala ya bunge hutekelezwa ndani ya bunge na wala sio nje hivyoba...