Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Maandamano Sudan: Vikosi vya jeshi vyazozana Khartoum



Baadhi ya wanajeshi wameanza kuwalinda waaandamanaji mjini Lkhartoum baada ya vikosi vya usalama kurusha vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji kulingana na mashahidi.

Wanajeshi walionekana wakijaribu kuyafukuza magari yaliokuwa yakijaribu kurusha vitoa machozi katika siku ya pili ya maandamano ya kutaka rais Omar al-Bashir kung'atuka uongozini.

Waandamanaji walionekana wakitafuta hifadhi katika kifaa cha jeshi la wanamaji huku wasiwasi kati ya majeshi ukioonekana wazi.

Bashir kufikia sasa amekataa kuondoka mamlakani ili kutoa fursa kwa serikali ya mpito. Maelfu ya waandamanaji wamekita kambi nje ya makao makuu ya jeshi nchini Sudan, wakimtaka rais Omar al-Bashir ajiuzulu.

Inavyoonekana wanatarajia mapinduzi ya ndani ya nchi, wakiliomba jeshi kumtimua Bashir na kufungua njia ya kupatikana serikali ya mpito.

Ni maandamano makubwa dhidi ya Bashir tangu kuzuka ghasia mnamo Desemba mwaka jana.


Bashir amekataa kuondoka, akieleza kwamba wapinzani wake wanastahili kutafuta uongozi kupitia uchaguzi. Jeshi halijaingilia kati.

Maafisa wa usalama wamefyetua gesi ya kutoa machozi kuwatimua wandamanaji nje ya makao hayo makuu katika mji mkuu, Khartoum.


Waandamanaji walipiga kelele "jeshi moja, watu wamoja" nje ya makao mkauu ya jeshi Sudan

Maandamano haya yanaadhimisha miaka 34 ya mapinduzi yaliouondoa utawala wa rais Jaafar Nimeiri.

Katika maandamano ya nyuma, wamettumia pia guruneti na silaha za moto zikiwemo risasi. waandamanaji kadhaa wameuawa .

Siku ya Jumamosi, mwandamanaji mmoja alifariki katika mji wa Omdurman, polisi wanasema.

Waziri wa habari nchini Sudan amethibitisha mipnago ya serikali kutatua mzozo kupitia mazungumzo na kupongeza vikosi vya usalama.

Ushindani wa kisiasa usiotarajiwa

Na Fergal Keane, Mhariri wa BBC Afrika

Ni wazi kwamba yanayodhihirika katika mji mkuu Khartoum yanardhirisha. Umati kama huuu haujawahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa.

Lakini kumeshuhudiwa vifo kadhaa na kuna uwezekano wa kuwepo msako mkali kwa hivi sasa.

Na hata iwapo rais Bashir atajiuzulu hakuna uhakika kwamba nafasi yake itachukuliwa na serikali itakayokuwa na uwakilishi wa wengi kama wanavyotaka waandamanaji.

Serikali za utawala wa nguvu katika karne ya 21 barani Afrika zimeadimika na kutoa taswira ya mabadiliko lakini inayotoa maana finyu.

Kinachofichuka sasa huenda ni sehemu ya ushindani wa kisiasa usiotarajiwa wa muda mrefu zaidi.

Je ni nini kinafanyika ndain ya vizuizi vya siri Sudan?

Ni kwanini watu wanaandamana?

Mwandishi habari Mohamed Ali Fazari, aliyekuwepo katika umati wa waandamanaji mjini Khartoum, anasema waanadamanaji hao wanaliomba jeshi lishirikiane na raia dhidi ya serikali.

Umati ulipiga kelele ukisema "uhuru, uhuru, haki - jeshi moja, watu wamoja", ameiambia BBC.

Kiini cha maandamano hayo awali kilitokana na gharama kubwa ya maisha lakini sasa ni ya kumshinikiza rais Bashir ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30 sasa, ajiuzulu.

Uchumi wa Sudan umeathirika kwa muda mrefu na vikwazo vya Marekani kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita inayoishutumu Khartoum kwa kufadhili makundi ya kigaidi.

Mnamo Desemba mwaka jana serikali ya Sudan ilitangaza kwamba bei ya mafuta na mkate itapanda

Katika mwaka uliofuata uamuzi huu, gharama ya maisha ilipanda huku pauni ya Sudan ikashuka thamani kwa kiasi kikubwa.

Tangazo la kupanda kwa bei ya bidhaa hizo ilichangia kuzuka maandamano, yaliogeuka kuwa shinikizo dhidi ya Bashir ajiuzulu.


Utawala wake umegubikwa kwa shutuma za uikukaji wa haki za binaadamu.

Mnamo 2009 na 2010, mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) ilimshtaki kwa makosa ya uhalifu wa kivita, mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binaadamu. Waranti wa kumkamata umetolewa.


Saturday's protests took place in cities all over Sudan

Rais amejibu nini?

Mnamo Februari , ilionekana ni kama atasalimu amri baada ya maandamano hayo na kjiuzulu, badala yake Bashir alitangaza hali ya dharura kitaifa.

Usalama umeimarishwa pakubwa mitaani huku gesi za kutoa machozi zikitumika kiholela na ripoti za kuwepo ghasia zikiwa ni jambo la kawaida.

Maafisa nchini humo wameshutumiwa kwa kuwakamata wanaharakati maarufu na kuwalenga matabibu , jambo ambalo idara ya ujasusi inakana.

Maafisa wanasema watu 32 wamefariki katika ghasia zinazohusiana na maandamano kufikia sasa, lakini shirika la Human Rights Watch linasema huenda idadi hiyo ni 51.

Kundi la kutetea haki za binaadamu Physicians for Human Rights linasema lina ushahidi wa mauaji, na unyanyasaji wa waandamanaji wa amani na matabibu waliokuwa wakiwashughulikia

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...