Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 6, 2016

Rais Magufuli ameweka nadhiri yake

MTEULE THE BEST RAIS MAGUFULI SIO WA MCHEZO KILA KUKICHA TANZANIA YAKE INAPIGA HATUA MBELE , RAIS MAGUFULI  RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania John Magufuli, ameweka mikakati imara.Hayumbishwi kwa kile anachokiiamini kuwa anafanya kwhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kiuchumi ambayo anaitekeleza kwa kasi kubwa    Moja ya mambo anayoyaamini kuwa yatasimamisha uchumi wa Tanzania nia pamoja na kujenga viwanda nchini.  Katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli tayari mfuko wa Pensheni wa PPF umeanza kutekeleza agizo hilo kwa kuingia ubia na jeshi la Magereza na kuanzisha kiwanda cha kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi Makubaliano haya yalisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza Bw.John Minja Octoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa makao Makuu ya Jeshi la Magereza uliopo Jijini Dar es Salaam. katika makubaliano hayo PPF itakarabati na kuboresha miundombinu ya kiwanda cha viatu cha karanga ambacho uzalish...

Tume za Haki za Binadamu kutoka nchi ya Kenya, Uganda na Burundi zakutana

MTEULE THE BEST Tume za Haki za Binadamu kutoka nchi ya Kenya, Uganda na Burundi zimekutana nchini Tanzania kujadili namna ambavyo tume hizo zinaweza kusimamia viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Utawala bora, amani na haki za binadamu. Akifungua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema mkutano huo utatoa tadhmni ya miaka 3 ya utendaji wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, sambamba na kutoa mapendekezo mapya kwa nchi hizo hasa katika kutatua migogoro na kulinda amani. Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Marry Massay amesema tume hizo zinawajibu wa kuhakikisha haki inazingatiwa, kutatua migogoro baina ya wananchi na viongozi wao na kushugulikia malalamiko. Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu kutoka nchini Burundi Jean Baribonekeza amesema hali ya Burundi kwa sasa imeimarika tofauti na mwaka mmoja ulipita ikiwa ni juhudi ya tum...

TRA IMEFANIKIWA KUSHINDA KESI 9 DHIDI YA WAKWEPA KODI NCHINI

MTEULULE THE BEST Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 zilizokuwa zikiendelea katika mahakama mbalimbali nchini dhidi ya walipa kodi wake na kufanikiwa kupata kiasi cha takribani Bilioni 16.9. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hali ya makusanyo na zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN)linaloendelea hivi sasa. “Tumefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 ambazo zilifikishwa mahakamani dhidi ya walipa kodi na kupata kiasi cha shilingi bilioni 16.9 hivyo kufanya juhudi zetu za kukusanya mapato mengi zaidi” Aliongeza Kayombo. Katika hatua nyingine Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikia kukusanya shilingi trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba ikiwa ni kukamilisha malengo waliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato. “Tumefanikiwa kukusanya shilingi Trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa ni kufanikisha maleng...

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amevifutia usajili vyama vya siasa

MTEULE THE BEST Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi  Dar es Salaam.  Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi  amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutowasilisha ripoti za ukaguzi wa hesabu za fedha. Sababu nyingine ni kutokuwa na ofisi na kushindwa kuthibitisha kuwa na wanachama Zanzibar Amevitaja vyama hivyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta) kilichokuwa kinaongozwa na James Mapalala na The Progressive Party of Tanzania (APPT-Maendeleo) kilichokuwa kinaongozwa na Peter Mziray kama Rais Mtendaji. Chama kingine kilichofutiwa usajili ni Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na Kassim Bakari kama Mwenyekiti taifa Source: Mwananchi

Obama ampongeza Trump, amwalika White House

MTEULE THE BEST   Rais  Obama amempigia simu Donald Trump kumpongeza kwa ushindi uchaguzi wa urais ambapo pia amemwalika ikulu ya White House mnamo Alhamisi wajadiliane kuhusu shughuli ya mpito. Obama pia amempigia Hillary Clinton na kumpongeza kutokana na alivyofanya kampeni. Rais Obama atatoa taarifa zaidi Jumatano kutoka White House kujadili matokeo ya uchaguzi na hatua ambazo tunaweza kuchukua kama taifa kuungana tena pamoja baada ya kipindi cha uchaguzi huu uliokuwa na ushindani mkali", katibu wa ikulu amesema kupitia taarifa. Taarifa kamili hii hapa:

TRUMP:- WASOMALI WANAEEZA ITIKADI KALI

MTEULE THE BEST Image Mgombea wa urasi nchini Marekani Donald Trump asema jamii ya Wasomali nchini Marekani inaenneza itikadi kali Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ameishambulia jamii ya Wasomali wanaoishi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani ,akiwalaumu kwa kueneza maoni yenye itikadi kali nchini humo. Alitumia mfano wa kisa cha shambulio la kisu lililotekelezwa na mhamiaji raia wa Somalia mnamo mwezi Septemba katika mji wa St.Cloud ,akisema kuwa wakaazi wa Minnesota wameteseka vya kutosha. Bwana Trump ambaye alikuwa katika ziara ya kampeni kabla ya uchaguzi wa Jumanne amesema kuwa iwapo atakuwa rais atahakikisha kuwa wakaazi wa maeneo wanashauriwa kabla ya wakimbizi kupelekwa ili kuishi. Clinton atabahatika mara ya pili? Obama amtaka Trump kuacha kulalama Hivi ndivyo alivyosema Trump: "Viongozi wetu wana ujinga kiasi gani? Wana Ujinga kiasi gani kuruhusu mambo kama haya kutokea? Hapa Minnesota mumekabiliwa na matatizo chu...