MTEULE THE BEST
RAIS MAGUFULI SIO WA MCHEZO KILA KUKICHA TANZANIA YAKE INAPIGA HATUA MBELE ,
RAIS MAGUFULI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania John Magufuli, ameweka mikakati imara.Hayumbishwi kwa kile anachokiiamini kuwa anafanya kwhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kiuchumi ambayo anaitekeleza kwa kasi kubwa
Moja ya mambo anayoyaamini kuwa yatasimamisha uchumi wa Tanzania nia pamoja na kujenga viwanda nchini.
Katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli tayari mfuko wa Pensheni wa PPF umeanza kutekeleza agizo hilo kwa kuingia ubia na jeshi la Magereza na kuanzisha kiwanda cha kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi
Makubaliano haya yalisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza Bw.John Minja Octoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa makao Makuu ya Jeshi la Magereza uliopo Jijini Dar es Salaam.
katika makubaliano hayo PPF itakarabati na kuboresha miundombinu ya kiwanda cha viatu cha karanga ambacho uzalishaji ulianza mwaka 1977 na kufunguliwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Maoni