TRA IMEFANIKIWA KUSHINDA KESI 9 DHIDI YA WAKWEPA KODI NCHINI

MTEULULE THE BEST

Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 zilizokuwa zikiendelea katika mahakama mbalimbali nchini dhidi ya walipa kodi wake na kufanikiwa kupata kiasi cha takribani Bilioni 16.9.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hali ya makusanyo na zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN)linaloendelea hivi sasa.

“Tumefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 ambazo zilifikishwa mahakamani dhidi ya walipa kodi na kupata kiasi cha shilingi bilioni 16.9 hivyo kufanya juhudi zetu za kukusanya mapato mengi zaidi” Aliongeza Kayombo.

Katika hatua nyingine Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikia kukusanya shilingi trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba ikiwa ni kukamilisha malengo waliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato.

“Tumefanikiwa kukusanya shilingi Trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa ni kufanikisha malengo ya ukusanyaji kodi nchini ili kukuza uchumi wa nchi pamoja kusaidia Serikali kuendeleza huduma za jamii nchini” Alisema Kayombo.

Aidha Kayombo amesema kuwa mapato hayo yametokana na mikakati thabiti iliyowekwa na mamlaka hiyo katika ukusanyaji kodi hapa nchini ili kuweza kusaidia ongezeko la Pato la Taifa .

Mbali na hayo Kayombo amesema kuwa zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi ambalo limeanza hivi karibuni linaendelea na litafikia tamati Novemba 30 mwaka huu kwa mkoa Dar es salaam hivyo wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya uhakiki huo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU