Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amevifutia usajili vyama vya siasa

MTEULE THE BEST

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi 

Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi  amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutowasilisha ripoti za ukaguzi wa hesabu za fedha.

Sababu nyingine ni kutokuwa na ofisi na kushindwa kuthibitisha kuwa na wanachama Zanzibar

Amevitaja vyama hivyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta) kilichokuwa kinaongozwa na James Mapalala na The Progressive Party of Tanzania (APPT-Maendeleo) kilichokuwa kinaongozwa na Peter Mziray kama Rais Mtendaji.

Chama kingine kilichofutiwa usajili ni Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na Kassim Bakari kama Mwenyekiti taifa

Source: Mwananchi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU