Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MADURO

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro Marekani inapanga njama ya kumuua na kupindua serikali yake

John Bolton amepewa jukumu la kupanga jinsi ya kuniangamiza' Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akizungumza na wanahabari mjini Caracas Desmba 12,2018 Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amedai kuwa Marekani inapanga njama ya kumuua na kupindua serikali yake. Amewaambia wanahabari kuwa mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani John Bolton, anahusuka moja kwa moja na njama hiyo japo hakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo. Rais Trump amemtaja Maduro kama kiongozi wa kiimla na kumwekea vikwazo. Mapema wiki hii maafisa wakuu wa Urusi na Marekani walijibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini. Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumatatu katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo. Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia. Madur...