WAJUMBE NANE WA KAMATI KUU CHADEMA WATUMBULIWA

Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini leo Mei 13, 2025 imetengua uteuzi wa wajumbe 8 wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walioteuliwa baada ya kikao cha Baraza Kuu la Taifa cha tarehe 22 Januari 2025 siku moja tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa chama hiko. Kwa mujibu wa chanzo cha ndani cha Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa amefanyia kazi malalamiko ya Lembrus K. Mchome kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 4(5)(a)na(b) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 na Kanuni ya 31(2)(3) ya Kanuni za Usajili na Ufuatiliaji wa Vyama vya Siasa za Mwaka 2019 (Political Parties (Registration and Monitoring) Regulations, 2019 GN. 953) amebaini kuwa malalamiko ya Mchome ni ya ukweli kwamba kikao cha Baraza Kuu la Taifa la CHADEMA kilichofanyika tarehe 22 Januari 2025 kilikuwa batili, kwa sababu kilikuwa hakina akidi inayotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya Mwaka 2006 toleo la 2019. Vilevile, hata kama kikao hicho. Ameomgeza kuwa hata kama kikao ...