HADI hapo , nilitaka kutoa picha tu ya mafundisho tusiyoyasomea ambayo baadhi yetu wameshajiingiza katika kufundisha . Lakini , kwa nini tunafanya hivyo ? Bila shaka, sababu ni tatu : mosi , kutokujua mafundisho ya Kanisa Katoliki ni yapi ; pili , kutekwa na vyama vya kitume au vikundi vya dini visivyojali wala kujua mafundisho ya Kanisa Katoliki na tatu , ni tatizo la kumkubali bwana wa pili , ndiye pesa (Mt 6:24). Mintarafu, kutokujua mafundisho ya Kanisa Katoliki ni yapi ni aibu. Ni aibu kwa padri aliyeandaliwa kuwa mwalimu katika Kanisa kutokujua kitu. Ni aibu kuketishwa chini na kufundishwa mambo batili na kishapo kuinuka yeye mwenyewe kufundisha mambo yasiyo ya Kanisa lake. Tuseme, basi “tumeliwa akili” na wapagani, Wapentekoste, Waislamu na kadhalika. Inakuaje tuache mafundisho ya kwetu nasi tutumikie dini au makanisa mengine? Inakuwaje sisi tulioandaliwa kuwa walimu tugeuzwe kuwa wanafunzi na wale tuliotazamiwa ku...