Wapiganaji nchini Somalia
Mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa la msalaba mwekundu raia wa Ujerumani ametekwa nyara katika mji mkuu wa Somalia.
Habari zinasema watu wasiofahamika waliokuwa wamebeba silaha, walimteka ndani ya eneo la ofisi hizo mjini Mogadishu na kumtoa nje kwa kutumia mlango wa nyuma, ili kuweza kuwakwepa walinzi waliokuwa katika lango kubwa la mbele.
Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu amesema wana wasiwasi mkubwa na usalama wa mfanya kazi mwenzao.
Amesema muuguzi huyo aliyetekwa alikuwa akifanya kazi kila siku kuokoa maisha ya baadhi ya Wasomali wenye hali mbaya
Maoni