MJUE DR. LOUIS SHIKA HISTORIA YA MAISHA YANGU NILIPOKUWA URUSI KAMA NILIVYOSIMULIA NIKIWA GLOBAL PUBLISHERS,SEHEMU YA 1 Dkt. Louis Shika ambaye amepata umaarufu mkubwa baada ya kushiriki katika mnada wa nyumba za Said Lugumi jijini Dar es Salaam na baadaye ‘kukwaruzana’ na jeshi la polisi kutokana na mchakato wa mnada huo, amefunguka engi kuhusu maisha yake. Katika simulizi hiyo, Dkt Shika ambaye hivi sasa ni maarufu kama ‘900 Itapendeza’ kutokana na mambo yaliyojiri katika mnada huo, alianza kwa kusema kwamba neno ‘daktari’ linalotangulia jina lake ni la kitaalam, yaani kweli yeye ni daktari wa binadamu akiwa alisomea taaluma hiyo nchini Urusi. “Nilisomea utaalam huo nchini Urusi nilikokwenda mwaka 1984 kwenda kuchukua digrii ya kwanza ya miaka saba ambayo niliimaliza mwaka 1991,” anasema daktari huyo mwenye mwili wa kiasi na kimo kirefu. Anaendelea kusema kwamba mwaka huohuo aliamua kuunganisha masomo apate digrii ya pili ya mag...