Trump akaidi uamuzi wa bunge na kuamua kuiuzuia silaha Saudi Arabia zenye thamani ya $8bn Rais Trump, akiwa pamoja na mwanamfalme wa Saudia wanashika chati inayoonyesha mauzo ya silaha kwa Saudia Rais huyo wa Marekani ametumia kura ya turufu kufutilia mbali uamuzi wa bunge la Congress la kuzuia mauzo ya silaha yenye thamani ya $8bn kwa Saudia na UAE. Donald Trump alisema kuwa maamuzi hayo matatu yatadhoofisha uwezo wa Marekani ulimwenguni na kuharibu uhusiano wake na washirika wake . Hatua hiyo inajiri baada ya mabunge yote mawili kupiga kura ya kuzuia mauzo hayo. Baadhi ya wabunge wanasema kwamba walihofia kwamba silaha hizo huenda zikatumiwa dhidi ya raia katika mgogoro wa Yemen. Wameshutumu vitendo vya Saudia nchini Yemen pamoja na mauaji ya mwaka jana ya mwandishi Jamal Khashoggi. Hatahivyo bunge le seneti litapiga kura baada ya siku moja ili kuona iwapo litakaidi uamuzi wa bwana Trump , kulingana na kiongozi wa wengi katika chama cha Republican Mitch Connel. Lakin...