Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 24, 2016

Jeshi la Sudan kusini na tuhuma nzito

MTEULE THE BEST Shirika la Amnesty International limevituhumu vikosi vya serikali ya Sudan Kusini vimeua, kubaka na kuwateka raia. Shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa makubaliano ya amani. Ripoti hiyo, imetaja muda wa matukio hayo kuwa ni kati ya mwezi Agosti mwaka 2015 na Disemba 2015, kipindi ambacho vijiji pia vilichomwa moto. Zaidi ya watu milioni mbili wamekimbia makazi yao nchini Sudan Kusini tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka miwili iliyopita. Ripoti hiyo inagusia ukiukwaji ambao umeathiri mtu mmoja mmoja na vijiji katika nchi ya Sudan Kusini. Amnesty inasema imefanya mahojiano na watu walioshuhudia wanaume kwa wanawake wakipigwa risasi na makundi yaliyokuwa yakishambulia. Baadhi ya watoto na wazee wanaripotiwa kuchomwa moto wakiwa hai huku watoto wa kike wakibakwa mfululizo. Mashuhuda wanasema, wanajeshi walivalia sare za jeshi pindi walipovamia. Katika siku zilizopita, Umoja wa Ma...

Gonzalo anunuliwa kwa pauni milioni 75

MTEULE THE BEST Juventus wamemnunua mshambuliaji wa Agentina Gonzalo Higuain kutoka Timu ya Napoli kwa pauni milioni 75.5 Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa miaka mitano baada ya Juventus kukubali kutoa kitita hicho kinachokaribia Euro milioni 90 ambazo watazilipa kwa awamu. Malipo hayo ya Mzaliwa wa Ufaransa Higuain aliyeanzia uchezaji wake wa kulipwa katika timu ya River Plate ya Argentina yanachukua nafasi ya tatu kwa ukubwa baada ya yale yaliyolipwa na Real Madrid walipomnunua Cristiano Ronaldo kwa Pauni milioni 80 na Gareth Bale kwa Pauni milioni 85.

Bill Clinton: "mke wangu" Hillary anafaa kuwa rais

MTEULE THE BEST Image copyright AP Image caption Bw Clinton amemweleza mkewe kama"rafiki mkubwa" Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amemsifu sana mkewe Hillary na kusema anafaa kuongoza taifa hilo. Ameambia kongamano kuu la chama cha Democratic mjini Philadelphia kwamba mkewe ndiye “mfumaji bora zaidi niliyewahi kukutana naye”. Kwenye hotuba yenye hisia kali, amemweleza Hillary kama “rafiki mkubwa” na akasimulia walivyokutana na jinsi anavyojitolea katika utumishi wa umma. Saa chache awali, mkewe aliibuka kuwa mwanamke wa kwanza nchini Marekani kuidhinishwa kuwania urais na chama kikubwa Bi Clinton alihitimisha shughuli za usiku huo wa Jumanne kwa ujumbe wa video ambapo alisema: “Siamini kwamba tumefanikiwa kuweka ufa mkubwa zaidi katika dari hili la kioo”, akirejelea hotuba ya mkewe Rais Barack Obama, Michelle, siku ya kwanza ya kongamano. “Na iwapo kuna wasichana wadogo huko ambao hawajalala na wananitazama, ningependa kuwaambia, huenda nikawa rais ...

Tazama Hotuba Nzito ya Rais Magufuli Baada ya Kukabidhiwa Ccm

MTEULE THE BEST

Speech ya Jacklin Wolper akirudi CCM Mbele ya Jakaya na Mzee Kinana.

MTEULE THE BEST

WOLPER AIKACHA CHADEMA DUH AZAMIA CCM KIROHO SAFI WATU WATOKWA MAPOVU JI...

MTEULE THE BEST

MREMA: KAMA MIMI NI CCM B BASI LOWASSA NI CCM A

MTEULE THE BEST

Wazaramo wakifanya mapenzi kwenye gari huku wakicheza Ngoma

 Wazaramo wakifanya mapenzi kwenye gari huku wakicheza Ngoma MTEULE THE BEST

Helicopter iliyotengenwa Mkoani Songwe ilivyovuta watu wengine kwenye ma...

 Helicopter iliyotengenwa Mkoani Songwe ilivyovuta watu wengine kwenye ma...  MTEULE THE BEST

RIWAYA: JERAHA LA HISIA SEHEMU YA SITA

MTEULE THE BEST RIWAYA: JERAHA LA HISIA MTUNZI: George Iron Mosenya Mawasiliano: 0655 727325 SEHEMU YA SITA KIMBOKA, ni moja ya baa maarufu sana jijini Dar es salaam. Umaarufu wake si kwa sababu ya huduma bora wanazotoa ama mandhari nzuri ya kuvutia katika baa hiyo. Umaarufu wake ulisambaa sana kutokana na huduma ya bei rahisi pengine kuliko sehemu yoyote katika jiji hilo. Huduma ambayo inawasaidia makapela azidi kusahau kuhusu ndoa mathalani kuishi na mwanamke ndani. Biashara ya uuzaji miili kwa bei nyepesi sana. Baa hii ilikuwa makazi ya mwanadada Naomi kwa kipindi tangu akimbie shutuma za kuhusika katika kifo cha Maureen. Naomi alikimbilia huku si kwa kuwa naye alikuwa wa bei rahisi sana kwa wakati huo la. Alihofia usalama wake na kubwa zaidi alikuwa amechanganyikiwa. Dawa ya kutuliza mawazo aliamini kuwa ni kunywa pombe, basi kama kweli ni pombe Kimboka zinapatikana kwa bei ya kawaida bila nyongeza yoyote. Naomi akawa Naomi wa Kimboka. Dada yake naye alikuwa kitu kingine ...

RIWAYA: JERAHA LA HISIA SEHEMU YA TANO.

MTEULE THE BEST RIWAYA: JERAHA LA HISIA MTUNZI: George Iron Mosenya Mawasiliano: 0655 727325 SEHEMU YA TANO. "Ulale pema peponi Maureen, msalimie bibi mwambie mchumba wangu Naomi sijui alipo, wasalimie baba na mama waambie nawapenda sana, kwaheri dada Maureen"Aliongea hayo Walter wakati anauaga mwili wa Maureen uliokuwa umepondekapondeka vibaya kutokana na majanga aliyoyapata, kwanza umeme halafu ajali mbaya ya gari. Maneno na sauti yake vilimchoma kila mtu aliyeyasikia,Walter alikuwa na jeraha kisogoni, nguo zake zilikuwa chafu sana. Hakuhitaji kubadilisha na hakuwepo wa kuweza kumshawishi lolote. "Nilitegemea kula nawe sikukuu za mwisho wa mwaka kwa nini hukusubiri lakini! Mbona hukutaka walau nipate dakika mbili za kukuona ukitabasamu. Ewe ardhi mwenye tamaa nimeze na mimi uridhike, hivi baba na mama hawakukutosha? Bibi naye je…haya na dadangu umemchukua….eeh Ardhi nimeze sasa hivi niondoke na Maureen" alishindwa kujizuia Walter akaangua kilio kikali...

RIWAYA: JERAHA LA HISIA SEHEMU YA TATU

MTEULE THE BEST RIWAYA: JERAHA LA HISIA MTUNZI: George Iron Mosenya Mawasiliano: 0655 727325 SEHEMU YA TATU Naomi hakuwa na pombe kichwani, akili zilikuwa timamu kabisa,alikuwa anatetemeka sio kwa baridi bali uoga mkubwa sana,alikuwa amekodoa macho macho yake, akili ilimruhusu kwenda mbele lakini miguu ikiwa mizito kama amevaa viatu vya chuma.Jasho likamtoka licha ya mvua iliyokuwa imenyesha. * * * * Jeuri ya pesa aliyokuwa nayo ilimpelekea Dj Walter kufanya manunuzi ya bei ghali sana kwa fujo, alikuwa na furaha kubwa sana kurejea Tanzania kushehereke sikukuu za mwisho wa mwaka pamoja na familia yake. Lakini furaha yake kubwa ilikuwa maendeleo mazuri kiafya ya dada yake Maureen. Gari yake mpya aina ya Land Cruiser Prado ilikuwa imechafuka kwa mapochopocho. Malipo mazuri aliyokuwa akilipwa yalimfanya Walter awe mmoja kati ya watu maarufu na wenye fedha nchini Uganda lakini hakulewa sifa aliendelea kuwa karibu na Anko Muga na sasa walikuwa naye ndani ya gari wakisafiri ...

Wabunge wa Ujerumani wataka wahamiaji waliokataliwa wafukuzwe haraka

MTEULE THE BEST Wabunge wa Ujerumani wataka wahamiaji waliokataliwa wafukuzwe haraka Wabunge wa Ujerumani wametoa mwito wa kuharakishwa kwa mchakato wa kuwafukuza wahamiaji wanaokataliwa hifadhi nchini Mji wa Ansbach baada ya mashambulio ya Jumapili Mbunge wa chama kinachoongoza serikali ya mseto CDU, Armin Schuster amesema Ujerumani inapasa pia kuwa na tabia ya kusema kwaheri, na sio ya kukaribisha tu. Bwana Schuster ameeleza katika mahojiano na magazeti muhimu ya nchini Ujerumani kwamba Ujerumani imeshindwa kuitekeleza kanuni ya kuwafukuza haraka wahamiaji, baada ya maombi yao ya kuishi nchini kukataliwa. Bwana Schuster ambae pia ni mtaalamu wa masuala ya ndani ya nchi bungeni, amefahamisha kwamba bado wapo wahamiaji zaidi ya laki nchini Ujerumani, ingawa maombi yao ya kuishi nchini yamekataliwa. Naye Mbunge wa chama cha mrengo wa kushoto Sarah Wagenknecht ameikosoa sera ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel juu ya wakimbizi. Amesema matukio ya siku za ...

Bernie Sanders na Michelle Obama wampigia debe Hillary Clinton

MTEULE THE BEST Bernie Sanders na Michelle Obama wampigia debe Hillary Clinton Vigogo miongoni mwa vigogo wa chama cha Democratic cha Marekani, Michelle Obama na Bernie Sanders wameshangiriwa walipohutubia mkutano mkuu wa chama chao na kusema Hillary Clinton anastahiki kuwa rais wa Marekani . Katika wakati ambapo uchunguzi wa maoni ya umma unamtaja Donald Trump kumpita Hillary Clinton katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha rais wa Marekani,mke wa rais wa sasa wa Marekani Michelle Obama amewasisimua umati wa wafuasi wa Democrats waliohudhuria mkutano mkuu wa Philadelphia alipokosoa tabia ya Trump na kusifu dhamira ya kumkabidhi madaraka mwanamke awe rais wa Marekani kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo. Wito wa Michelle Obama ulikuwa wa kuleta suluhu na wa dhati na ulipokelewa vyema na umati wa watu waliohudhuria kikao cha ufunguzi cha mkutano mkuu huo wa siku nne. Baada ya kumsifu na kuzungumzia uwezo na sio rangi wala kabila Michelle Obama amesema...

Kombe la dunia: Afrika kuongezwa nafasi 2 zaidi

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Image copyright GETTY Image caption Rais wa shirikisho la soka duniani Infantino Bara la Afrika litatunukiwa nafasi nyengine mbili zaidi iwapo dimba la dunia litaongeza idadi ya mataifa yanayoshiriki hadi 40 kuanzia mwaka 2026 kulingana na rais wa FIFA Gianni Infantino. Infantino alipendekeza kuongezwa kwa timu hizo kabla ya kuchaguliwa kwake na shirikisho hilo la soka duniani. Kwa sasa Afrika ina nafasi tano pekee katika michuano hiyo . ''Pendekezo langu limekuwa timu 40 na iwapo hilo litadhinishwa pendekezo langu ni kulipatia bara la Afrika nafasi mbili zaidi'',alisema Infantino. Hatahivyo hatua hiyo itaidhinishwa hadi mwaka 2026 huku timu 32 zikiwa tayari zimethibitishwa kushiriki katika kombe la dunia la 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qatar.

Lyon yakataa ombi la Arsenal kumnunua Lacazette

MTEULE THE BEST Lyon yakataa ombi la Arsenal kumnunua Lacazette Image copyright AP Image caption Mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette Klabu ya Lyon imekataa ombi la Euro milioni 35 kutoka Arsenal kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alifunga mabao 21 katika mechi 34 msimu uliopita na kandarasi yake katika klabu hiyo inakamilika 2019. Katika taarifa yake katika mtandao wa Twitter,Klabu hiyo ya Ufaransa ilisema Lacazette hanunuliki na ni miongoni mwa viongozi wa timu hiyo ya kocha Bruno Genesio. Lyon ilikana ripoti ya gazeti moja kwamba ilikataa ombi la Euro milioni 48 kutoka kwa klabu hiyo ya Uingereza.

Jux - Wivu (Official Music Video)

JUX: WIVU MTEULE THE BEST

Treni ya mwendo wa kasi yazinduliwa Nigeria

MTEULE THE BEST Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria leo ameanzisha rasmi usafiri wa treni za kisasa zilizo na uwezo wa kuendeshwa kwa mwendo wa kasi. Mradi huo wa kwanza kwa Nigeria umeigharimu nchi hiyo dolla million $850 .Reli hizo za kisasa kwa mfumo uitwao standard gauge(SGR) zilijengwa na kampuni kutoka Uchina. Reli hizo ambazo ni mbili kwa moja yaani moja ni ya kwenda na nyengiine ya kurudi, zinaunganisha miji ya Abuja na Kaduna ambapo treni zitaweza kusafiri kwa mwendo wa kasi ya kilomita 120 hadi 150 kwa saa. Wakati wa ufunguzi wa leo rais Buhari mwenyewe amesafiri kwa treni hiyo hivyo kuuanzishwa mfumo huo wa usafiri wa reli kwa umma. Nauli kutoka mji huo mkuu wa Nigeria Abuja hadi mji wa Kaduna ulioko jimbo la kazkazini mwa nchi hiyo ni dolla $1:50 pekee. Awali mradi huo ulikumbwa na chelewa chelewa za kisiasa baada ya kunzia utawala wa Obasanjo, ukapitia utawala wa Yardua hadi utawala wa Goodluck Jonathan na ndio sasa umekamilika tayari kwa matumizi katika utaw...