MTEULE THE BEST
Wanaume wa wanawake kutoka Kenya ndio warefu zaidi eneo la Afrika Mashariki kwa wastani kwa mujibu wa utafiti ambao matokeo yake yametolewa leo.
Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la eLife yanaonesha kimo cha wastani miongoni mwa wanaume wa Kenya ni sentimeta 169.64 na wanaume sentimeta 158.16.
Utafiti huo ndio wa kina zaidi kufanywa, kwa mujibu wa watafiti hao, na uliangazia matokeo kutoka utafiti 1,472 uliofanywa katika mataifa 200.
Ulifuatilia kimo cha watu waliozaliwa mwaka 1896 hadi wale waliozaliwa mwaka 1996 ambao walitimiza umri wa miaka 18 mwaka 1914 hadi mwaka 2014. Waliochunguza kote duniani ni watu 18.6 milioni.
Kimo cha watu hutegemea lishe anayopata mama akiwa mjamzito pamoja na lishe ya mtoto anapokuwa mchanga.
Kimo cha mtu huhusishwa sana na afya ya mtu kwa jumla pamoja na hali ya maisha.
Watu warefu kwa kawaida huishi maisha marefu na huwa hawana matatizo mengi ya moyo na kupumua.
Utafiti huo wa kimo unaonesha Waafrika waliongeza urefu hadi kufikia miaka ya 1960 na 1970 lakini baada ya hapo wakaanza kupunguza kimo.
Watafiti waliohusika, miongoni mwao James Bentham na Majid Ezzati wa Chuo cha Imperial cha London, Uingereza, wanasema huenda hili limetokana na kusambaratika kwa mifumo ya afya, ongezeko la idadi ya watu na kubadilika kwa lishe hasa kutokana na watu wengi kuhamia mijini.
Ikizingatiwa kwamba ni kipimo cha wastani, kuwepo kwa watu wachache warefu sana katika baadhi ya nchi huenda kiliathiriwa na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wafupi.
Kimo cha wastani katika mataifa ya Afrika Mashariki na mataifa mengine ya karibu, kwa mujibu wa utafiti huo, ni kama ifuatavyo:
Wanaume (kimo cha wastani kwa sentimita) Wanawake (kimo cha wastani kwa sentimita)
Kenya 169.64 158.16
Burundi 166.64 154.02
Uganda 165.62 156.72
Tanzania 164.80 155.86
Rwanda 162.68 154.79
Zimbabwe 168.57 158.22
Sudan 166.63 156.04
Ethiopia 166.23 155.71
DR Congo 166.80 155.25
Congo Brazaville 167.45 157.57
Zambia 166.52 155.82
Malawi 162.23 154.40
Msumbiji 164.80 153.96
Wanaume (kimo cha wastani kwa sentimita) | Wanawake (kimo cha wastani kwa sentimita) | |
Kenya | 169.64 | 158.16 |
Burundi | 166.64 | 154.02 |
Uganda | 165.62 | 156.72 |
Tanzania | 164.80 | 155.86 |
Rwanda | 162.68 | 154.79 |
Zimbabwe | 168.57 | 158.22 |
Sudan | 166.63 | 156.04 |
Ethiopia | 166.23 | 155.71 |
DR Congo | 166.80 | 155.25 |
Congo Brazaville | 167.45 | 157.57 |
Zambia | 166.52 | 155.82 |
Malawi | 162.23 | 154.40 |
Msumbiji | 164.80 | 153.96 |
Maoni