MTEULE THE BEST
Juventus wamemnunua mshambuliaji wa Agentina Gonzalo Higuain kutoka Timu ya Napoli kwa pauni milioni 75.5
Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa miaka mitano baada ya Juventus kukubali kutoa kitita hicho kinachokaribia Euro milioni 90 ambazo watazilipa kwa awamu.
Malipo hayo ya Mzaliwa wa Ufaransa Higuain aliyeanzia uchezaji wake wa kulipwa katika timu ya River Plate ya Argentina yanachukua nafasi ya tatu kwa ukubwa baada ya yale yaliyolipwa na Real Madrid walipomnunua Cristiano Ronaldo kwa Pauni milioni 80 na Gareth Bale kwa Pauni milioni 85.
Maoni