MTEULE THE BEST
Shirika la Amnesty International limevituhumu vikosi vya serikali ya Sudan Kusini vimeua, kubaka na kuwateka raia.
Shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa makubaliano ya amani.
Ripoti hiyo, imetaja muda wa matukio hayo kuwa ni kati ya mwezi Agosti mwaka 2015 na Disemba 2015, kipindi ambacho vijiji pia vilichomwa moto.
Zaidi ya watu milioni mbili wamekimbia makazi yao nchini Sudan Kusini tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka miwili iliyopita.
Ripoti hiyo inagusia ukiukwaji ambao umeathiri mtu mmoja mmoja na vijiji katika nchi ya Sudan Kusini.
Amnesty inasema imefanya mahojiano na watu walioshuhudia wanaume kwa wanawake wakipigwa risasi na makundi yaliyokuwa yakishambulia.
Baadhi ya watoto na wazee wanaripotiwa kuchomwa moto wakiwa hai huku watoto wa kike wakibakwa mfululizo.
Mashuhuda wanasema, wanajeshi walivalia sare za jeshi pindi walipovamia.
Katika siku zilizopita, Umoja wa Mataifa pia umewahi kulishutumu jeshi la Sudan Kusini na makundi yanayoshirikiana nayo kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Hata hivyo, serikali ya Sudan Kusini imekana vikosi vyake kuhusika na tuhuma hizo.
Ingawa chama tawala na waliokuwa waasi wamesaini makubaliano ya amani na kuunda serikali ya pamoja, lakini bado kuna hali ya wasiwasi baina yao.
Hali hii imeonekana hivi karibuni katika mauji yaliyofanyika mjini Juba.
Riek Machar ambae yuko upinzani nafasi yake ya ukamu wa rais imechukuliwa na aliyekuwa mshirika wake wa karibu Taban Deng Gai.
Maoni