mteulethebest Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema wajibu wa kuiendeleza Afrika uko mikononi mwa Waafrika wenyewe huku jukumu la wadau wengine wa Maendeleo ni kusaidia kukua kwa Maendeleo hayo. Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo Leo katika Mahafali ya Programu za ESAMI yaliyofanyika katika Makao Makuu ya ESAMI jijini Arusha ambapo amesisitiza kuwa Waafrika wanapaswa kujisimamia wenyewe katika nyanja za Kijamii na Kiuchumi kwa lengo la kutimiza malengo ya bara hilo. “ Ili Afrika iweze kuendelea lazima ijisimamie yenyewe katika masuala ya kijamii na kiuchumi na hii itawezekana tu kupitia vijana ambao wameandaliwa vyema na wakawa tayari kuhakikisha wanaliendeleza bara la Afrika kwa ujasiri bila kuhofia changamoto watakazokutana nazo,” alisisitiza Waziri Ndalichako Kiongozi huyo amesema bara la Afrika linahitaji Viongozi wenye ujasiri, ambao wapo tayari kuhakikisha Afrika inakwenda mbele kiuchumi na Kija...