Na Rahel Nyabali, Tabora
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji wote wa serikali kuwajibika kikamilifu kwa kusikiliza kero na kutatua changamoto kwa wananchi kwa kujituma.
Ameyasema hayo Wilaya ya Tabora Mkoani Tabora katika jukwaa la fursa biashara na uwekezaji na kuwataka wakuu wa Wilaya na watendaji kuwajibika vilivyo kwa kusimamia shuguli za serikali kikamilifu.
"Nachukua nafasi hii kwa kuwakumbusha ili kila mmoja akawajibike kwa nafasi yake kwa kutambua furssa zilizoko mahali husika kwa lengo la kuinua uchumi wa mmoja mmjo na taifa kwa ujumla ili kufikia uchumi wakati ifikapo 2025, amesema Majaliwa.
Majaliwa amesema Mkoa wa Tabora unafursa nyingi za uwekezaji hasa katika kilimo kwa mazao ya biashara na chakula kwa kutambua fursa hiyo mkoa huo utafanikiwa kuongeza pato la Taifa
"Mkoa huu una ardhi yenye rutuba unazalisha tumbaku kwa asilimia kubwa una asali alizeti na zao la korosho litaanza kupandwa muda Si mrefu hivyo wawekezaji inatakiwa wapate furusa ya pekee ili kuwekeza kwa wingi kwani kunaulinzi wa kutosha" amesema Majaliwa.
Aidha amezitaka Taasisi zote zinazo jihusisha na ulasimu kuacha malamoja pia zinatakiwa zikae eneo moja ili kupunguza mzunguko wa kupata vibali kwa wawekezaji na hatua zitachukuliwa kwa mtu yeyote au taasisi itakazo kwamisha wawekezaji kushindwa kuwekeza mkoani homo
Maoni