Raisi wa Marekani Donald Trump amesema jeshi la maji la Marekani limetungua ndege isiyo na rubani ya Iran katika eneo la mpaka kati ya ghuba ya uajemi na ghuba ya Oman. Amesema meli ya jeshi lake ''ilichukua hatua'' siku ya Alhamisi baada ya ndege hiyo kusogea kwa takriban mita 914 karibu na chombo hicho. Iran haijasema chochote kuhusu hilo. Mwezi Juni, Iran iliangusha ndege ya kijeshi isiyo na rubani ya Marekani, na kusababisha hofu ya kutokea mzozo wa kijeshi. Awali Tehran ilisema imekamata ''meli ya kigeni'' na wafanyakazi wake 12 siku ya Jumapili kwa kusafirisha mafuta kinyume cha sheria. Iran imekuwa ikishutumiwa na Marekani kwa kushambulia meli zake tangu mwezi Mei.Tehran ilikana shutuma hizo. Raisi Donald Trump amesemaje ? Akizungumza Ikulu, Trump amesema ''Ninataka kuwajulisha kuhusu tukio lililotokea kwenye eneo la mpaka wa Hormuz leo lililohusisha meli yetu ya kijeshi. Chombo hicho kilichukua hatua ya kujilinda dhidi ya nde...