Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MELI ZA KIVITA

Meli za Kivita za Urusi Zinafanya Mazoezi ya Kombora katika Bahari ya Japani

Meli za kivita za Urusi za Pacific Fleet zilifanya mazoezi ya pamoja ya kurusha risasi dhidi ya shabaha ya dhihaka katika Bahari ya Japan .   Picha zilizochapishwa na wizara ya ulinzi zinaonyesha meli mbili zikirusha makombora ya kusafiri ya Moskit na kufanikiwa kulenga shabaha yao kwa takriban kilomita 100 (maili 62).

MAREKANI YALIPIZA KISASI KWA IRAN

Raisi wa Marekani Donald Trump amesema jeshi la maji la Marekani limetungua ndege isiyo na rubani ya Iran katika eneo la mpaka kati ya ghuba ya uajemi na ghuba ya Oman. Amesema meli ya jeshi lake ''ilichukua hatua'' siku ya Alhamisi baada ya ndege hiyo kusogea kwa takriban mita 914 karibu na chombo hicho. Iran haijasema chochote kuhusu hilo. Mwezi Juni, Iran iliangusha ndege ya kijeshi isiyo na rubani ya Marekani, na kusababisha hofu ya kutokea mzozo wa kijeshi. Awali Tehran ilisema imekamata ''meli ya kigeni'' na wafanyakazi wake 12 siku ya Jumapili kwa kusafirisha mafuta kinyume cha sheria. Iran imekuwa ikishutumiwa na Marekani kwa kushambulia meli zake tangu mwezi Mei.Tehran ilikana shutuma hizo. Raisi Donald  Trump  amesemaje ? Akizungumza Ikulu, Trump amesema ''Ninataka kuwajulisha kuhusu tukio lililotokea kwenye eneo la mpaka wa Hormuz leo lililohusisha meli yetu ya kijeshi. Chombo hicho kilichukua hatua ya kujilinda dhidi ya nde...

Boti za Iran zajaribu kuzuiwia meli ya Uingereza kulipiza kisasi

Meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose imeripotiwa kuifukuza mbali maboti ya Iran Maboti ya Iran yaliyosheheni silaha yameripotiwa kujaribu kuzuwia safari ya meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la kuwa maji la Strait of Hormuz - kabla ya ya kufukuzwa na meli ya kikosi cha majini cha Uingereza. Taarifa za vyombo vya habari zimenukuu maafisa wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya mafuta iliambiwa isimame katika maji ya Iran yaliyopo karibu ,lakini ikarudi nyuma na kuondoka baada ya onyo kutolewa na mele ya jeshi ya Uingereza. Iran imekuwa ikitishia kulipiza kisasi kufuatia kushikiliwa kwa moja ya meli zake za mafuta ambayo ilitekwa karibu na ibraltar wiki iliyopita. Makao makuu ya wizara ya Ulinzi nchini Marekani Pentagon yamesema kuwa yanataarifa juu ya tukio hilo lakini hayakutoa taarifa zaidi. Kwa mujibu wa taarifa , boti tano zinazoaminiwa kumilikiwa na jeshi la Iran Iranian Revolutionary Guard ziliikaribia meli ya mafuta ya Uingereza ilipokuwa ikiondoka eneo la...