Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Boti za Iran zajaribu kuzuiwia meli ya Uingereza kulipiza kisasi





Meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose imeripotiwa kuifukuza mbali maboti ya Iran

Maboti ya Iran yaliyosheheni silaha yameripotiwa kujaribu kuzuwia safari ya meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la kuwa maji la Strait of Hormuz - kabla ya ya kufukuzwa na meli ya kikosi cha majini cha Uingereza.


Taarifa za vyombo vya habari zimenukuu maafisa wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya mafuta iliambiwa isimame katika maji ya Iran yaliyopo karibu ,lakini ikarudi nyuma na kuondoka baada ya onyo kutolewa na mele ya jeshi ya Uingereza.

Iran imekuwa ikitishia kulipiza kisasi kufuatia kushikiliwa kwa moja ya meli zake za mafuta ambayo ilitekwa karibu na ibraltar wiki iliyopita.


Makao makuu ya wizara ya Ulinzi nchini Marekani Pentagon yamesema kuwa yanataarifa juu ya tukio hilo lakini hayakutoa taarifa zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa , boti tano zinazoaminiwa kumilikiwa na jeshi la Iran Iranian Revolutionary Guard ziliikaribia meli ya mafuta ya Uingereza ilipokuwa ikiondoka eneo la Ghuba.


Ramani ya Straits of Hormuz na Bab al-Mandab ambapo meli ya mafuta ya Uingereza inadaiwa kukabiliwa na maboti ya ya Iran

Wakiwa na silaha juu ya meli ya kijeshi ya Uingereza -HMS Montrose, wanajeshi wa kikosi cha majini wa Uingereza waliripotiwa kuzilazimisha boti za Iran kurudi nyuma . Waliafiki onyo na hapakuwa na makabiliano yoyote ya silaha.

Wiki iliyopita, Kikosi cha wanamaji cha Uingereza- British Royal Marines kilisaidia maafisa wa Gibraltar kukamata meli ya mafuta ya Iran kutokana na ushahidi kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea kwenye mwambao wa Syria ambao uko chini ya maneneo yaliyowekewa vikwaza na Muungano wa Ulaya.

Afisa wa Iran alisema kuwa meli ya mafuta ya Ungereza lazima ikamatwe na kama ikikamatwa haiwezi kuachiliwa.


Iran pia ilimuita balozi wa Uingereza mjini Tehran kumlalamikia juu ya kile ilichosema kuwa ni "aina ya uharamia".

Na Jumatano rais wa Iran Hassan Rouhani aliikemea Uingereza, na kuitaja kama taifa lenye "uoga" na "lisilo na matumaini" kwa kutumia meli zake za kijeshi kuficha meli yake ya mafuta katika eneo la Ghuba.

meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose ilikuwa imeikinga meli ya mafuta Pacific Voyager ilipokuwa ikisafiri kuelekea katika maeneo ya Strait of Hormuz, lakini safari hiyo ilimalizika bila tukio lolote.

Meli ya mafuta inashukiwa kubeba shehehena ya mafuta ghafi kuelekea nchini Syria

Mzozo wa hivi karibuni unakuja wsakati hofu ikiendela kutandabaina ya Marekani na Iran

Utawala wa Trump ambao tayari umejiondoa kwenye makubaliano ya kimataifa juu ya mpango wa nuklia wa Tehran - umeimarisha vikwazo vya kuiadhibu Iran.

lakini washirika wa Ulaya, ikiwemo Uingereza, hawakufuata mkondo huo wa Marekani.


Hata hivyo, uhusiano baina ya Uingereza na Iran umeendelea kuzorota, baada ya utawala wa Iran ''ulipojaribu kushambulia meli mbili za mafutra za Uingereza mwezi Juni.

Uingereza pia imeishinikiza Iran kumuachiliwa huru mama Muingereza mwenye asili ya Iran Nazanin Zaghari-Ratcliffe ambaye alikamatwa mnamo mwaka 2016 baada ya kupatikana na hatia ya ujasusi, ambao anaukana.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...