Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TAA

TANROADS, TAA SHIRIKIANENI MIRADI YA KIMKAKATI IKAMILIKE KWA WAKATI

Picha
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameziagiza Taasisi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kumsimamia Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato ili mradi huo ukamilike kwa wakati na ubora. Amesisitiza Taasisi hizo kuwa na mawasiliano na ushirikiano wa karibu kwani Watanzania wanasubiria mradi huo na kuahidi yeye pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule kuukagua mradi huo mara kwa mara. Ulega ametoa maelekezo hayo Mkoani Dodoma mara baada ya kukagua utekelezaji wa mradi huo wa kimkakati ambao umefika asilimia 53.9 na kusisitiza kuwa ukikamilika unatarajiwa kuinua uchumi wa Mkoa wa Dodoma na kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji. “Nimekagua jengo hili la abiria ambalo ni la kisasa na Mkandarasi yupo nyuma ya muda, hivyo nimeagiza Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group na Hebei Construction Group Corporation (BCEG) afanye kazi usiku na mchan...