Mbwana Samatta: Sababu ya mshambuliaji wa Tanzania kung’ang’aniwa na klabu za West Ham, Everton na Burnley Englan
Mbwana Samatta: Sababu ya mshambuliaji wa Tanzania kung’ang’aniwa na klabu za West Ham, Everton na Burnley England Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta anang'ang'aniwa na klabu tatu za England, taarifa za vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema. Tetesi zinasema nyota huyo anatafutwa na West Ham United, Everton na Burnley. Samatta, 25, maarufu kwa Watanzania kama Samagoal ameng'aa sana akichezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji. Amefungia klabu hiyo mabao 11 katika mechi 16 ambazo amewachezea msimu huu, nusu ya mabao hayo akiyafunga barani Ulaya. Samatta asaidia klabu yake kufuzu Europa League Utafiti: Mbwana Samatta, Salim Kikeke wana ushawishi mkubwa Tanzania Kylian Mbappe ana uhusiano na Tanzania? Jedwali la Msimamo wa ligi ya EPL 2018/19 Taarifa za kumhusisha Samatta na klabu ya Everton zimetoka kwa mtandao wa hitc.com, mmoja wa mitandao ambayo imeibukia kuwa maarufu kwa taarifa za wachezaji na kuhama kwao. Kwa nini anahusishwa na ...