Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 24, 2018

Biashara ya shirika la ndege la Air Tanzania yaimarika

Biashara ya shirika la ndege la AIR Tanzania Company Limited (ATCL) imepanda thamani kwa kipindi cha miaka miwili licha ya kuwa na abiria wachache waliotumia ndege zake kusafiria Mkurugenzi wa biashara wa ATCL Patrick Ndekana aliambia gazeti la  D aily News  kwamba biashara za shirika hilo la serikali iliongezeka kutoka asilimia 2.5 mwaka 2016 hadi asilimia 42.6 mwisho wa mwaka jana huku ikiwa na ndege mbili pekee zinazofanya kazi. Amesema kuwa wana matumaini kwamba biashara hiyo itaimarika zaidi baada ya kununuliwa kwa ndege mpya. ''Mwaka huu biashara yetu itaongezeka hususan baada ya kuwasili kwa ndege ya tatu kubwa aina ya Bombadier Q-400s na baadaye kuwasili kwa Bombadier nyengine mbili za Cs 300s ambazo zitakuwa na viti vingi'', alisema. Kwa sasa shirika hilo linamiliki ndege tatu aina ya Q-400 katika maeneo 10 tofauti nchini, mbali na kuelekea Comoro. Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka jana, shirika hilo limekuwa likisafirisha abi...

Watu watano wauawa kwa shambulio la risasi Maryland Marekani

Polisi wakiimarisha usalama katika eneo la tukio Polisi katika jimbo la Maryland nchini Marekani wanasema watu watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la risasi lililofanyika katika ofisi za kampuni ya Capital Gazette inayomiliki magazeti ya kila siku katika mji wa Annapolis. Wafanyakazi wa gazeti hilo wanasema mshambuliaji huyo ambaye ni mzungu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 ambaye alijiharibu vidole vyake ili kuepusha kutambulika kwa alama za vidole alifyatua risasi hovyo kupitia mlango wa vioo. Tiyari amekamatwa na polisi. Rais Trump ametuma salam za rambirambi William Krampf ambaye ni Msaidizi mkuu wa polisi wa Anne Arundel amesema kwamba wamekuta pia vitu vilivyokuwa na muonekano wa vilipuzi na kuvidhibiti kwa haraka. Ameongeza kwamba watu zaidi ya 170 waliokuwa katika jengo hilo walisindikizwa na polisi katika kuhakikisha wanakuwa salama kutoka katika jengo hili ambalo pia lilikuwa na biashara nyingine. Kupitia mtandao wa twite...

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wafikia makubaliano kuhusu uhamiaji

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano juu ya mpango wa uhamiaji, unaozitaka nchi wanachama kwa hiari kuanzisha vituo vya udhibiti kushughulikia wahamiaji waliookolewa baharini na kuanzisha vituo nje ya ulaya. Mpango huo wa maelewano uliofikiwa mapema asubuhi ya leo unakuja baada ya majadiliano yaliyodumu kwa muda wa masaa zaidi ya 12, wakati viongozi hao walipokutana katikati mwa ongezeko la shinikizo la kutafuta ufumbuzi wa tatizo la uhamiaji, unaonekana kuhatarisha mustakabali wa umoja huo. Mpango huo ni ushindi kwa Italia, inayoongozwa na waziri mkuu Giuseppe Conte, ambaye amekuwa akisukuma ajenda ya kugawana mzigo wa wahamiaji miongoni mwa nchi wanachama na hata kutishia kutumia kura yake ya turufu katika maamuzi ya mkutano huo wa kilele hadi pale viongozi wake wangefikia makubaliano ya pamoja juu ya uhamiaji. "Kwa hiyo naweza kusema kwa ujumla tunaweza kuridhika. Yalikuwa majadiliano ya muda mrefu lakini kuanzia leo Italia haiko peke yake," alisema C...

Diamond Platinumz: Daylan ni mwanangu halisi 'msiniletee

Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz amewapuuzilia mbali wanaodhania kwamba yeye sio baba wa kweli wa mtoto wake wa kiume wa mwanamitindo Hamisa Mobetto. Diamond alichapisha ujumbe mkali katika mtandao wake wa Instagram akithibitisha kuwa Daylan ni mwanawe anayempenda sana. Hatua hiyo inajiri baada mwanamuzilki huyo kuchapisha kanda fupi ya video akivumisha ziara yake ya Marekani. Kanda hiyo fupi ya video inamuonyesha Diamond akizungumza kuhusu kazi yake na familia. Anazungumzia vile atakavyokuwa mbali na familia yake kwa takriban mwezi mmoja suala litakalomfanya kutowaona dada zake, mamake na watoto wake. Kanda hiyo ya video hatahivyo iliwaonyesha wanawe wawili aliyozaa na mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan. Video hiyo haikumuonyesha mwana wa Hamissa Mobetto, hatua iliowakera mashabiki wake waliotoa hisia tofauti kabla ya Diamond kuchapisha ujumbe huu. ''Huyu ni mwanangu... na ataendelea kuwa mwanangu maisha yangu yote, tena kipenzi changu... .Hakuweza kuwepo kweny...

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

Rais Mnangagwa wa Zimbabwe aizuru Tanzania kukuza uhusiano

Rais Mnangagwa alikaribishwa rasmi na mwenyeji wake rais John Magufuli Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa yuko Dar es salaam katika ziara ya kwanza nchini humo tangu aingie madarakani. Ni ziara ya siku mbili ambayo imetajwa kulenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mwenyeji rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na Rais Mnangagwa wamekubaliana kuimarisha biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili yaliotajwa kuwa na udugu wa kihistoria. Mnangagwa amewasili asubuhi hii na kupokewa na rais Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Akiwa Tanzania kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea chuo cha kilimo alikosomea miongoni mwa wapiganjiaji uhuru waliotoka nchi za kusini mwa Afrika. Kukuza uhusiano wa Zimbabwe na Tanzania: Tanzania ilikuwa na jukumu muhimu katika mataifa ya Afrika yaliojikomboa dhidi ya utawala wa wazung...

Simba yawajibu wanaobeza usajili wao

Klabu ya soka ya Simba imesema inafanya usajili kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi, matakwa ya timu na ushiriki wa mashindano kwa msimu ujao na si pesa walizonazo, au kulipa kisasi kwa watani zao Yanga kama inavyosemwa sasa. Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara. Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaama na Msemaji wa timu hiyo Haji Sunday Manara, wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi za timu hiyo. Manara amesema wachezaji waliokuwepo wamefanya kazi kubwa hivyo kwa hali ya msimu ujao wanahitaji watu wa ziada, wenye uzoefu kwaajili ya kuongeza nguvu zaidi. “Kwa wachezaji wa ndani ukimtoa Kaseja, Dida ndio golikipa aliyecheza mechi nyingi za kimataifa, hivyo Pascal Wawa amekuja kuziba pengo la Juuko aliye kwenda Afrika ya kusini kwa majaribio, Kagere tunaye kwasababu ya kuwasaidia Okwi na Bocco kila mtu anaujuwa uwezo wake” , a mesema Manara. Mpaka sasa Simba imekamilisha Usajili wa wachezaji sita wapya wane wa ndani na wawili wa kimat...

USAJILI:- ROONEY AJIUNGA NA DC UNITED

Everton na Wayne Rooney wamefikia makubaliano ya mchezaji kujiunga na MLS upande D.C. United kwa uhamisho wa kudumu. Mchezaji wa rekodi ya England atahamia Washington baada ya kufunga mabao 11 katika maonyesho 40 Everton baada ya kurudi kwenye Club kutoka Manchester United msimu uliopita. Mbele mwanzo alijiunga na Everton mwenye umri wa miaka tisa na alihitimu kupitia Chuo kikuu cha Blues kabla ya kufanya timu yake ya kwanza dhidi ya Tottenham Hotspur siku ya ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu ya 2002/03. Rooney akawa mchezaji mdogo zaidi wa Klabu wakati, mwenye umri wa miaka 16, alipiga mara mbili katika tiketi ya Ligi ya Ligi ya Wrexham mnamo Oktoba 2002 na wiki baadaye aliingia fahamu ya taifa kwa mgomo wa kushinda mechi ya klabu ya Arsenal ya England David Seaman. Kampeni yake ya kwanza aliona Rooney akifunga mabao sita kabla ya kushinda kofia yake ya kwanza ya Uingereza mwezi Februari 2003. Ujana wa Evertonian bado ni mchezaji mdogo sana wa Lions baada ya kupiga wavu dhidi ya Maked...

Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.

Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani. Alijipatia kipato cha $275m (£205m) katika mechi yake ya masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani. Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza katika kipindi cha miaka 2 iliopita sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua wadhfa wa pili kwa tofauti ndogo. La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake katika orodha hiyo baada ya mwanamke wa pekee katika orodha hiyo Serena Williams kutoorodheshwa. Wachezaji 100 bora walijipatia jumla ya $3.8bn, ikiwa ni nyongeza ya asilimia 23 kutoka mwaka uliopita ,Forbes ilisema Dereva wa magari ya F1 Lewis Hamilton ndio mwanamichezo Muingereza anayelipwa kipato cha juu cha $51m akiwa nambari 12. Mayweather ambaye jina lake la utani ni Money-aliongeza kipato chake cha michezo kwa $10m ...

Baba Mzazi wa Michael Jackson  aaga dunia

Baba mzazi wa aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson mzee Joe Jackson amefariki Dunia kwa ugonjwa wa Saratani (Cancer) akiwa na umri wa miaka  89 mapema Jumatano leo Baba mzazi wa aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson, Joe Jackson enzi za uhai wake. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka nchini humovimeeleza kuwa Bw. Jackson alikuwa akipambana na saratani ya kongosho . Inadaiwa kuwa kwa miaka mingi, Jackson ambaye alizaliwa Julai 26, 1928, huko Fountain Hill, Arkansas alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya afya. Joe alikuwa mzazi aliyefanikiwa sana kusimamia watoto wake katika historia ya muziki ambapo aliweza kujenga kundi la The Jackson 5, na kisha baadaye Michael na Janet Jackson kama wasanii solo. Amefariki dunia ikiwa imepita siku moja tangu kumbukumbu ya miaka tisa ya kifo cha mwanae Michael ambaye alifariki dunia Juni 25 2009. Jackson alikuwa na watoto 10 pamoja na Katherine ambaye ni mke wake wa zaidi ya miaka 60. 

Mtandao wa JamiiForums wafunguliwa tena Tanzania

Mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Maxence Melo Jukwaa maarufu nchini Tanzania JamiiForums hatimaye limefunguliwa baada ya kufungwa kwa takriban wiki mbili, kufuatia kuanza kutekelezwa kwa sheria mpya za mtandaoni nchini humo. Kulingana na ujumbe uliosambazwa katika ukurasa wa Twitter wa tovuti hiyo, kwa sasa ujumbe ambao ulikuwa umepakiwa awali unaweza kusomwa. Mkurugenzi wa mtandao huo Maxence Melo aliyekuwa akijibu ujumbe wa mmoja wa wateja wake katika mtandao wa Twitter amenukuliwa katika ujumbe huo akisema hata hivyo kwamba watumiaji wa mtandao huo hawawezi kuchapisha ujumbe mpya kwa sasa. Aliongezea kusema kwamba hatua za kurejesha operesheni zote kama ilivyokuwepo mwanzo zinaendelea. Kwa sasa habari za mtandao huo ambazo zilikuwa zimechapishwa kuanzia 10 Juni kwenda nyuma kabla ya kufungwa kwa jukwaa hilo zinaweza kusomwa. Hata hivyo haijajulikana ni lini operesheni kamili za mtandao huo zitaanza ili wasomaji kuanza kuchangia. Walipofunga mtandao huo...

Licha ya ukuta, 11 wakamatwa wizi wa Tanzanite

Watuhumiwa 11 wamekamatwa na jeshi lapolisi kwa wizi wa madini ya Tanzanite yenye gramu 1110 yenye thamani  ya Tsh 5,551,234.92 yaliyoko ndani ya ukuta wenye kilo meter 24.5 uliojengwa kwenye mgodi wa 'Tanzanite one' ulioko Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Madini ya Tanzanite (Picha ya mtandaoni) Kamanda wa polisi mkoani humo Agustino Senga akizungumza na waandishi wa habari amethibitisha kuibiwa kwa madini hayo na kusema kuwa  watuhumiwa hao wameshafikishwa mahakamani Aidha Kamanda Senga amesema kwamba kwa sasa wanafanya tathmini ya kukagua migodi isiyotumika ili iweze kufungwa kutokana na kuwa migodi hiyo ndiyo inayotumika kuwa njia  ya kuingilia kwenye migodi yenye madini. Aidha Kamanda Senga amefafanua kuwa madini hayo yameibiwa na wachimbaji wadogo wadogo na wafanyakazi wa mgodi huo wa 'Tanzanite One' ambao wanauzoefu na mazingira ya maeneo hayo hivyo hutumia uzoefu wao kwa kutengeneza njia za panya maarufu kama mtobozano. Madini hayo yali...

Msichana apambana na malaria kwa mishumaa

Yumkini sasa ugonjwa hatari wa malaria unaweza ukawa historia nchini Tanzania, kutokana na mbinu mbalimbali zinazoibuliwa na wananchi wa kawaida kukabiliana na ugonjwa huu sugu katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Serikali imekuwa ikifanya juhudi katika kukabiliana na malaria kwa kunyunyizia dawa za kuuwa viluwiluwi vinavyosababisha ugonjwa huo kwenye makaazi ya watu, kugawa vyandarua vyenye dawa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujikinga na ugonjwa huu.  Licha ya jitihada hizi kusaidia, lakini tatizo la msingi bado liliendelea kuwapo. Nalo ni uwelewa mdogo wa walengwa kwenye kampeni yenyewe. Lakini sasa matumaini ya kutokomeza malaria yamezaliwa upya baada ya kutengenezwa kwa mishumaa inayofukuza mbu, hatua itakayoongeza nguvu katika juhudi za kupambana na ugonjwa huu. Beatrice Mkama ni mjasiriamali mwenye ndoto za kuisaidia jamii yake katika kuitokomeza malaria iliyosababisha kuondokewa na ndugu zake waliofariki baada ya kuugua ugonjwa huo. Beatrice, ambaye kitaaluma...

“Samaki wana maumbile kama Binadamu”- Musukuma

Mbunge wa Geita vijijini (CCM), Joseph Musukuma amesema kuwa samaki wako wa aina tofauti Ziwani na wengine wana tabia kama binadamu kwa kile alichodai wana maumbile madogo lakini wana umri mkubwa. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma akichangia Bungeni Musukuma ametoa kauli hiyo bungeni leo, wakati akihoji swali la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu kwa wizara ya mifugo na uvuvi ambapo amesema kuwa suala la kupima kwa rula samaki haliafiki kwa kuwa viumbe hao pia wana maumbile tofauti kama binadamu. “ Dhana ya uvuvi haramu imeenea sana, lakini samaki pia wana maumbile tofauti kama binadamu na mfano ukichukua umri wangu mimi na mheshimiwa Mwalongo tunalingana lakini ukitutazama maumbile tunatofautiana sana, sasa hata samaki wako hivyo, kwahiyo hata samaki wakipimwa kwa rula hawalingani, sheria haijalitazama hilo, Je ni lini sheria itamtazama mvuvi na kumlinda pindi anapokumbana na changamoto hii ya samaki kuwa na maumbile tofauti na umri wake ?”,...

Ndugai awachimba mkwara Wabunge wa 'hapana'

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewatahadharisha Wabunge wake kwamba endapo wataipigia kura ya hapana Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, Rais atalivunja Bunge hilo huku akiwakumbusha wengine wanaweza wasirudi kwenye mjengo huo. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiwakumbusha wabunge kazi waliyonayo leo itakapofika saa 11 jioni  ambayo itakuwa kupiga kura ya kuipitisha bajeti. “Endapo mlio wengi mtaikataa Bajeti ya Serikali, bunge hili Rais atalivunja haraka. Na baadhi yenu, mkirudishwa majimboni hamrudi kwa hiyo akili za kuambiwa changanya na zako .” amesema Spika Ndugai. B Mbali na hayo Ndugai amewasisitiza wabunge wote kuwapo bungeni ifikapo saa 11  na kuwakumbusha kuwa kura haipigwi kwa jambo moja, bali ni kwa mfuko wote wa bajeti. Wabunge wanatarajia kupigia kura bajeti ambapo Serikali inatarajia kukusanya na kutumia TSh32...

Somalia: Mwanamume afunga ndoa na wanawake wawili wakati mmoja

Mohamed na wake zake wawili Kijana mmoja raia wa Somalia ambaye alioa wanawake wawili usiku mmoja ameambia BBC kwamba atawashawishi wanaume wengine kufanya hivyo. Bashir Mohamed anasema kuwa aliwachumbia wanawake wote kwa takriban miezi minane na kuwashawishi kufunga ndoa naye. ''Nilikuwa nikiwaleta nyumbaji wote pamoja'', aliambia BBC. ''Nilikuwa nikiwaambia wazi wote wawili kwamba nawapenda. Waliridhika'' , aliongezea. ''Umuhimu wa kuwaoa wote wawili wakati mmoja ni kwamba hawangekuwa na wivu na kwamba watajua tangu awali kwamba wamekuwa katika ndoa za uke wenza'', alisema bwana Mohammed. Alioa wanawake wawili kwa sababu alihitaji watoto wengi. ''Nitawashawishi wanaume wengi pia kufuata nyayo zangu iwapo wana uwezo'', alisema Mohamed. Ndoa za wake wengi ni halali katika utamaduni nchini Somalia lakini sio jambo la kawaida kuoa wanawake wawili wakati mmoja, kulingana na mwandishi wa BBC Mo...

Tanzania yakiri kuwa na Chikungunya, Dengue

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto nchini Tanzania imekiri kuwepo kwa magonjwa wa homa ya Chikungunya na Dengue katika taifa hilo kubwa kabisa Afrika Mashariki. Akitoa taarifa kwa wadau na waandishi wa habari mapema leo (Juni 25), Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amebainisha kuwa mnamo tarehe 20 Juni wasafiri wanne wa familia moja waliotokea Mombasa, Kenya, walibainika kuwa na ugonjwa huo kwenye kituo cha mpakani cha Holili, mkoani Kiliamanjaro. Awali jumla watu sita walibainika mwezi wa Januari mkoani Tanga kuwa na ugonjwa wa Chikungunya kupitia kwenye kituo cha mpakani cha Horohoro wakitokea pia Mombasa. Wakati huo huo, Tanzania imethibitisha pia kuwepo kwa homa ya Dengue, ambapo hadi sasa watu 226 wamethibitika kuwa na ugonjwa huo katika mkoa wa Dar es Salaam pekee, ambao ni kitovu cha kiuchumi na biashara.  Kwa mara ya kwanza homa ya Dengue iliripotiwa nchini humo mwaka 2010

Mazungumzo ya amani kati ya Ethiopia na Eritrea

Ujumbe wa ngazi ya juu wa serikali ya Eritrea unatarajiwa kuwasili katika nchi jirani ya Ethiopia kwa mazungumzo kuhusu juhudi za amani na kufufua matumaini ya kumalizika ugonvi uliodumu muda mrefu kabisa barani Afrika. Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema mapema mwezi huu yuko tayari kutekeleza masharti yote ya makubaliano ya amani  ya mwaka 1998-2000 yaliyomaliza ugonvi wa nchi hizo mbili, akiashiria uwezekano wa kupatiwa ufumbuzi mvutano kuhusu mpaka wa nchi hizo mbili. Rais Isaias Afwerki wa Eritrea akasema wiki iliyopita, anakaribisha kile alichokiita "risala za maana" kutoka Ethiopia na kuamua kutuma ujumbe wa kwanza rasmi wa serikali yake kuwahi kwenda Addis Abeba baada ya kupita miongo miwili . Ujumbe wa Eritrea unawaleta pamoja mshauri wa rais Yemane Gebreab, waziri wa mambo ya nchi za nje Osman Saleh na mwakilishi wa Eritrea katika Umoja wa Afrika-hayo ni kwa mujibu wa kituo cha matangazo kinachomilikiwa na serikali nchini Ethiopia. Wanajeshi ...

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte asema Mungu ni 'mpumbavu'

Duterte anafahamika kwa kutamka maneno ya kuzua ubishi Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amemwita Mungu "mpumbavu", hatua ambayo imekera sana watu katika taifa hilo lenye Wakatoliki wengi. Kiongozi huyo amesema hayo kwenye hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga. Aidha, amekosoa vikali hadithi ya Adam na Hawa kuhusu jinsi walivyotenda dhambi na kuondolewa kutoka kwenye neema ya Mungu. Kadhalika, amekosoa wazo kwamba kila binadamu tangu wakati huo huzaliwa akiwa na dhambi asilia. Bw Duterte anajulikana sana kwa matamko yake yenye kuzua utata pamoja na matusi yenye kutumia lugha kali dhidi ya wapinzani wake. ' Ingawa kanisa na raia wamemshutumu kwa hilo, afisi ya rais huyo imesema alikuwa tu anaeleza imani yake binafsi. Rais huyo amewahi kumshutumu pia Papa kwa kutumia maneneo makali na ana historia pia ya kuwatusi viongozi wengine. Tamko la sasa alilitoa katika hotuba mji wa Davao, mji ambao alikuwa kiongozi wake kabla ya kuwan...

Sera ya uhamiaji ya Ulaya itamfaa Merkel au Seehofer?

Mkutano mdogo wa kilele ambao ulioandaliwa Brussels kujadili sera ya uhamiaji na uliofanyika kwa ombi la Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye alikuwa kwenye shinikizo nchini mwake, haukutoa maamuzi yoyote. Lakini hotuba za viongozi wa nchi 16 waliohudhuria zinaashiria safari inakoelekea. Swali ni iwapo hatua zilizopangwa kuchukuliwa zitamsaidia Merkel katika mzozo na Waziri wake wa mambo ya ndani Horst Seehofer au iwapo mwanasiasa huyo wa chama cha Christian Social Union, CSU, atanufaika zaidi. Seehofer anasisitiza suluhisho la muda mfupi la wanaotafuta hifadhi kukataliwa kuingia Ujerumani wanapofika mpakani. Angela Merkel naye matumaini yake ya suluhisho ni maafikiano yatakayotokana na mazungumzo baina ya nchi kuhusu suala la kuwarudisha wahamiaji hao walikotoka. Mkutano huo wa Brussels ulitoa mapendekezo kadhaa na je mapendekezo haya yatakuwa na athari gani kwa siasa za ndani za Ujerumani? Baadhi ya nchi zinataka kubuniwe vituo vya mapokezi ya wakimbizi Libya ...

Raia wa Ghana bado hawafaidiki na ukuaji wa uchumi wake

Fedha ya Ghana iitwayo cedi ni miongoni mwa sarafu zenye nguvu Afrika Mamilioni ya raia wa Ghana bado hawafaidiki na ukuaji wa uchumi unaotajwa kuwa wa kasi nchini humo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa. Ripoti hii ni matokeo ya utafiti uliofanywa kwa siku kumi nchini humo, ikiangalia hali ya mabadiliko ya maisha sambamba na masuala ya haki ya binaadam. Ghana inatajwa kama miongoni mwa nchi zinazokua kiuchumi kwa kasi zaidi duniani, huku tegemeo kubwa likiwa kwenye sekta ya mafuta sambamba na zao la kakao. Rais Nana Addo aliingia madarakani 2017 akilenga kupambana na rushwa nchini humo Lakini kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa, mafanikio hayo yanawatajirisha matajiri pekee, huku asilimia kubwa ya wananchi ikisalia kutopea katika dimbwi kubwa la umaskini. Katika ripoti hiyo iliyoandaliwa na mwandishi wa umoja wa mataifa anayeshughulikia haki za binaadam sambamba na kuangalia hali ya umaskini Philip Alston, inasema asilimia 28 ya watoto bado ...

Mnangagwa:Uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa

Mnangagwa amesema uchaguzi uko palepale Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa tarehe 30 mwezi Julai, ingawa kulitokea alichokiita jaribio la kukatiza uhai wake lililotokea siku ya Jumamosi. Katika hatua nyingine, msemaji wa Polisi, Charity Charamba amevitaka vyombo vya habari na Umma kujitokeza iwapo wana picha za video za tukio la mlipuko wakati huu ambapo uchunguzi unafanyika. Amwewaambia wanahabari mjini Harare kuwa zawadi nono itatolewa kwa taarifa itakayotolewa kusaidia kwenye uchunguzi wao.Idadi ya waliojeruhiwa sasa imefika 49 na Polisi na idara za usalama ziko katika uwanja wa White City eneo ambalo mlipuko ulitokea. Watu walijeruhiwa kutokana na mlipuko uliotokea kwenye mkutano wa hadhara mjini Bulawayo, tukio lililotokea karibu kabisa na Mnangagwa wakati akiondoka jukwaani. Maafisa wamesema masuala ya usalama yataangaliwa tena. mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa ni wa kwanza tangu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo R...

Watu wawili wapoteza maisha baada ya mlipuko wa bomu nchini Ethiopia

Maelfu walikusanyika kwenye mkutano wa Waziri mkuu Abiy Ahmed Maafisa nchini Ethiopia wamesema kuwa watu wawili wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa, baada ya mlipuko wa bomu kutokea kwenye mkutano wa kisiasa wa Waziri mkuu, Abiy Ahmed. Bwana Abiy amelitaja shambulio hilo kuwa ''jaribio lililoshindwa la vikosi ambavyo havitaki Ethiopia iungane''. Kiongozi huyo aliondolewa mara tu baada ya mlipuko, unaoelezwa wa guruneti linaloaminika kurushwa kati ya maelfu ya watu katika viwanja vya Meskel , mjini Adis Ababa Naibu mkuu wa Polisi mjini humo anashikiliwa kutokana na kushindwa kusimamia hali ya usalama katika eneo hilo. Maafisa wa polisi wanane wanashikiliwa na wakihojiwa kwa kushindwa kulilinda eneo lilofanyiwa mkutano Waziri wa afya nchini Ethiopia aliandika kwenye akaunti yake ya twitter kuwa watu wawili wamepoteza maisha na wengine 44 wako hospitalini, watano kati yao wakiwa na hali mbaya sana. Abiy alikuwa Waziri Mkuu baada ya...

Wanawake wa Saudi Arabia waanza kuendesha magari

Jumapili hii imekuwa ya kihistoria kwa wanawake wa Saudi Arabia Wanawake nchni Saudi Arabia rasmi sasa wameruhusiwa kukaa kwenye usukani, baa ya miongo kadhaa kutopata ruhusa hiyo Mabadiliko haya yalitangazwa mwezi Septemba mwaka jana na Saudi Arabia ikatoa leseni za kwanza kwa wanawake mwanzoni mwa mwezi huu. Ilikuwa nchi pekee iliyobaki duniani ambapo wanawake walikuwa hawaendeshi magari na familia zao zilikuwa zinakodisha dereva kwa ajili ya wanawake. Hata hivyo, hatua hii imefikiwa wakati kukiwa na Kampeni ya kuwakamata wanaharakati ambao wamekuwa wakipaza sauti wapatiwe haki ya kuendesha magari. Takriban wanaharakati wa haki za wanawake wanane wanashikiliwa na huenda wakafikishwa mahakamani na kupatiwa kifungo kwa uanaharakati wao, Shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International limeeleza. Miongoni mwa wanaoshikiliwa ni pamoja na Loujain al-Hathloul, mwanaharakati kinara katika kampeni hiyo. Amnesty pia imetaka kufanyiwa mabadiliko makubwa ...