Fedha ya Ghana iitwayo cedi ni miongoni mwa sarafu zenye nguvu Afrika
Mamilioni ya raia wa Ghana bado hawafaidiki na ukuaji wa uchumi unaotajwa kuwa wa kasi nchini humo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa.
Ripoti hii ni matokeo ya utafiti uliofanywa kwa siku kumi nchini humo, ikiangalia hali ya mabadiliko ya maisha sambamba na masuala ya haki ya binaadam.
Ghana inatajwa kama miongoni mwa nchi zinazokua kiuchumi kwa kasi zaidi duniani, huku tegemeo kubwa likiwa kwenye sekta ya mafuta sambamba na zao la kakao.
Rais Nana Addo aliingia madarakani 2017 akilenga kupambana na rushwa nchini humo
Lakini kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa, mafanikio hayo yanawatajirisha matajiri pekee, huku asilimia kubwa ya wananchi ikisalia kutopea katika dimbwi kubwa la umaskini.
Katika ripoti hiyo iliyoandaliwa na mwandishi wa umoja wa mataifa anayeshughulikia haki za binaadam sambamba na kuangalia hali ya umaskini Philip Alston, inasema asilimia 28 ya watoto bado wanaishi katika umaskini uliotopea.
Philip Alston amesema ukuaji wa uchumi haugusi raia wote wa Ghana kwa sababu serikali bado haijafanya jitihada za kutosha kupunguza umaskini.
Serikali ya Ghana imeshauriwa kupambana na rushwa sambamba na matumizi mazuri ya kodi
Maoni